StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 7, 2012

FAHAMU UNDANI WA SAKATA LA MIPAKA ZIWA NYASA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Tanzania yaipiga marufuku Malawi
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2012/13.

Tanzania  imeapa kulinda mipaka yake kwa gharama yoyote na kuzionya ndege zozote za makampuni yanayofanya utafiti wa mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa kuruka kwenye anga la ziwa hilo, kuanzia jana.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alitangaza onyo hilo bungeni jana alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2012/13.

Waziri Membe alitoa kauli hiyo kufuatia taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Patrick Kabambe, ya wiki iliyopita kwamba ziwa hilo linamilikiwa na nchi yake kwa asilimia 100.

Kabambe alikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akieleza kwamba hawana sababu ya kusitisha utafiti wa mafuta na gesi kwa kuwa Malawi ndiye mmiliki wa ziwa Nyasa.

Hata hivyo, mikataba ya kimataifa na mipaka ya wakoloni inaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi upo katikati ya ziwa hivyo asilimia 50 ya ziwa hilo ipo Tanzania.

Membe alisema tatizo lililopo ni kwamba Malawi wanadai kuwa mpaka baina yake na Tanzania unapita pwani ya ziwa hilo; hivyo ziwa lote kutoka kwenye mpaka kati ya Malawi na Msumbiji hadi Kyela, Tanzania ni mali ya nchi hiyo.

Alisema Malawi wanajenga hoja kwa kuangalia mkataba uliowekwa na Waingereza na Wajerumani mwaka 1890 wa Anglo-German Agreeement ulioweka mpaka kati ya Tanzania na pwani ya Malawi.

Alisema Tanzania kwa upande wake inadai kwamba mpaka unapita katikati ya Ziwa kutoka mpaka wa Malawi na Msumbiji usawa wa latitudi nyuzi 9 na 11 hivyo kufanya eneo lote la Kaskazini Mashariki kuwa mali ya Tanzania.

Alisema Tanzania inazo ramani na mipaka iliyotengenezwa na wakoloni wa Kiingereza waliotawala Tanganyika na Malawi ambao walikubaliana kurekebisha mpaka na hivyo kuusogeza hadi katikati ya ziwa kama ilivyo kwa Malawi na Msumbiji.

Alisema baada ya kuibuka kwa tofauti hizo, ilikubalika kwamba pande zote zikutane ili kumaliza mgogoro huo kwa njia ya diplomasia.

Alisema tatizo la mpaka kwa Tanzania si la kwanza na katika mengine imefanikiwa kuyamaliza ikiwemo ule wa bahari kati yake na Comoro na Msumbiji, ambao ulimalizika Desemba mwaka jana.

Alisema mpaka mwingine ni ule uliobadilishwa Februari 17, mwaka huu, ambapo Tanzania ilikaa na Ushelisheli na pande zote zilibalisha mpaka wa Tanzania baharini.

Alisema katika mgogoro wa Malawi, madai ya Tanzania yanakuwa na nguvu kwa sababu ya kulinganisha mzozo kati ya Cameron na Nigeria kuhusu mpaka wa ziwa Chad ambao ulipelekwa Mahakama ya Kimataifa (International Court of Justice) na kuamuriwa kuwa mpaka huo upite katikati ya ziwa Chad katika mstari ulionyooka.

Alisema uamuzi huo ulitokana na sheria za kimataifa zinazoeleza pamoja na mambo mengine kwamba mstari ulionyooka upitao katikati ya ziwa ndio mpaka halali kati ya nchi na nchi ikiwa zitapakana na ziwa.

”Kutokana na maelezo haya yote, ni dhahiri kuwa tunalo tatizo linalohitaji kutatuliwa kati yetu na Malawi juu ya mpaka wa ziwa Nyasa,” alisema Membe.

Alisema tatizo la mpaka kati ya nchi hizo mbili lisingeweza kutatuliwa miaka ya nyuma kwa kuwa kiongozi wa Malawi wakati huo, Dk. Kamuzu Banda alikuwa rafiki wa serikali ya makaburu wa Afrika Kusini wakati Tanzania ilikuwa ikiunga mkono harakati za wapigania ukombozi wa watu weusi waliokuwa wakidai uhuru nchini humo.

Alisema Tanzania pia ilikuwa makao makuu ya vyama vya wapigania haki duniani hivyo wapinzani wa Malawi walikimbilia Tanzania jambo lililomfanya Banda aamini kwamba Tanzania ilikuwa kichaka cha maadui wa serikali yake.

”Haya hayakuwa mazingira mazuri ya kutatua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi kwa wakati huo,” alisema.

Membe alisema baada ya utawala wa Banda kuondoka, utawala wa Bakili Muluzi, Bingu wa Mutharika na sasa Joyce Banda, umeimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Malawi umeimarika kiasi cha kuruhusu majadiliano ya kumaliza mgogoro huo.

Alisema mwaka 2005, Mutharika alimwandikia Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akimtaka waunde kamati ya kuangalia tatizo hilo ili kulipatia ufumbuzi.

Alisema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani, alikutana na Mutharika mara mbili na wakakubaliana kuanzisha tume za kushughulikia tatizo hilo chini ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo.

Alisema timu ziliundwa na zilianza kukutana tangu mwaka 2010 na kuandaa hadidu za rejea kwa ajili kushughulikia tatizo hilo la mpaka ikiwemo kukusanya nyaraka mbalimbali.

Membe alisema mazungumzo yalikuwa yanaendelea, lakini katika hali ya kushangaza, Serikali ilipata taarifa za kuaminika kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwamba serikali ya Malawi imetoa eneo lote la ziwa Nyasa kama vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi.

Aidha, alisema makampuni yanayofanya utafiti huo ziliomba kibali cha kurusha ndege zake lakini Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilikataa.

”Pamoja na katazo hilo, serikali yetu ilipata ushahidi kwamba ndege ndogo za utafiti, zenye uwezo wa kutua majini na nchi kavu zinazokadiriwa kuwa tano zilionekana zikivinjari na kutua ziwa Nyasa katika upande wa Tanzania na kwenye ufukwe wake hayo yametokea kati ya Januari 29 na Julai 2, mwaka huu,” alisema.

Alisema: “Baada ya majadiliano ya makubwa baina yetu na Malawi, serikali yetu iliwataka wenzetu wa serikali ya Malawi pamoja na kampuni za utafiti au uchimbaji kusitisha mara moja shughuli zote za utafiti hadi majadiliano yatakapokamilika.”

Alisema baada ya matukio hayo, Tanzania iliwasiliana na serikali ya Malawi kwa maandishi na kuita mkutano wa kujadili hali hiyo na mustakabali wa mpaka huo uliofanyika Julai 27 na 28 jijini Dar es Salaam na pande zote zilikubaliana kwamba lipo tatizo baada ya kila mmoja kushikilia msimamo wake.

Alisema walikubaliana kwamba mkutano wa wataalamu na baadaye wa mawaziri wa mambo ya nje ufanyike nchini Malawi ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Alisema serikali ya Tanzania iliitaka serikali ya Malawi kutoruhusu kampuni yoyote kuendelea na utafiti kwa kuwa kufanya hivyo kungeathiri majadiliano.

”Serikali ya Tanzania inathamini uhusiano uliopo baina ya nchi mbili na ina dhamira ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema kwa manufaa ya watu wetu,” alisema.

Aliitaka serikali ya Malawi kuheshimu makubaliano ya Julai 27, mwaka huu kwa kuwa nia nzuri ya kutatua mgogoro baina yao ni mazungumzo ya amani.

Aliionya Serikali ya Malawi kutoruhusu mtu, kikundi au kampuni yoyote kufanya utafiti au uchimbaji kaskazini mwa ziwa Nyasa kwa kuwa majadiliano ya mpaka yanaendelea.

Alisema kuna Watanzania takribani 600,000 wanaotegemea ziwa Nyasa kiuchumi na kama chanzo cha uhai wao hivyo serikali itawalinda.

”Serikali ya Tanzania inapenda kuyaonya na kuyataka makampuni yote yanayofanya shughuli za utafiti kwenye eneo hilo linalobishaniwa kuanzia leo Jumatatu (jana), kuacha shughuli zao, serikali haitaruhusu utafiti huu kuendelea hadi makubaliano na majadiliano kuhusu mpaka yatakapofikiwa kati ya nchi zetu, tuipe diplomasia nafasi,” alisema.

Waziri Membe aliwataka wananchi wanaozunguka ziwa Nyasa kuendelea na shughuli zao za kiuchumi bila wasiwasi wowote kwa kuwa serikali iko macho, ipo imara na ipo tayari kulinda mipaka kwa gharama yoyote.

”Chini ya uongozi wa serikali ya CCM wananchi wa Tanzania daima watakuwa salama dhidi ya tishio lolote la dhahiri au la kificho la kiusalama, tumefanya hivyo tokea uhuru na hatutachelea kufanya vinginevyo wakati wote tukiwa madarakani,” alisema.

Hata hivyo, alisema upo uwezekano mkubwa wa mgogoro huo kutatuliwa na msuluhishi badala ya Tanzania na Malawi.
Wakati Membe akitoa taarifa hiyo,  na ujumbe wa kamisheni ya utumishi wa Bunge la Malawi, ulioongozwa na Naibu Spika wa Bunge hilo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere.

Septemba mwaka jana, aliyekuwa Rais wa Malawi, hayati Bingu wa Mutharika, aliridhia kampuni ya Surestream Petroleum ya Uingereza, kupewa leseni ya kufanya utafiti wa mafuta na gesi kwenye kina kirefu cha ziwa hilo na tayari kampuni hiyo imeanza kufanya utafiti wa athari za mazingira za mradi huo.

Ziwa Nyasa lina ukubwa wa kilometa za mraba 29,600 ambalo ni la tatu kwa ukubwa kati ya maziwa ya maji baridi barani Afrika.


UPANDE WA MALAWI WAJIBU HIVI:

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Malawi, Patrick Kabambe alikaririwa na Redio Sauti ya Ujerumani jana jioni akisema kuwa wataendelea na utafutaji wa mafuta na gesi katika Ziwa Malawi huku akidai kwamba amesikia Tanzania inapeleka askari eneo hilo.

Waziri huyo alisema hilo ni Ziwa Malawi na siyo Nyasa na kueleza kuwa utafutaji wa mafuta na gesi utaendelea na hakuna wa kuwasimamisha huku akihoji Tanzania kuja juu sasa na si wakati mwingine.

“Tutaendelea kutafuta mafuta na gesi katika Ziwa Malawi na tunashangaa kwa nini sasa ndiyo wanalalamika na siyo wakati mwingine?” alikaririwa akisema.

Geita gold Mine: Wafanyakazi waungana kupinga sheria mpya ya mafao ya SSRA- II

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Katibu wa TAMICO tawi la GGM Wilaya ya Geita na Kanda ya Ziwa, Shigela Alyce (aliyeshika kinaswa sauti ) akiwaongoza viongozi mbalimbali wa vyama vya wafayanyakazi pamoja na wafanyakzi kuimba wimbo wa solidarity forever (Mshikamano) mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara kupinga sheria mpya ya mafao ya SSRA , mkutano ambao ulifanyika mjini Geita kwenye uwanja wa Magereza
millionfortune.com
Wafanyakazi mbalimbali wa kampuni za mgoni wa GGM wakiwa mabango katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Magereza mjini Geita

millionfortune.com wafanayakazi geita wapinga sheria ya mafao
Wafanyakzi wa migodini na sekta binafsi wakimsikiliza Katibu wa TAMICO Wilaya ya Geita, Shigela Aloyce, hayupo pichani , wakati akihutuibia kwenye uwanja wa Magereza Geita Jumamosi, kupinga sheria ya mafao ya SSRA

DAH, MAJAMBAZI WANUSURIKA KIFO!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Kijana mtuhumiwa wa wizi wa piki piki Mohamed akivuja damu kwa kichapo na akiandaliwa kuchomwa moto kabla ya kuokolewa na polisi
Polisi wakimwokoa mtuhumiwa wa wizi wa piki piki
Mke wa mtuhumiwa akichezea kichapo kwa wizi
 
Mtuhumiwa wa pili wa wizi wa piki piki
mtuhumiwa wa wizi wa piki piki Mohamed Chambogo akichezea kichapo
Hapa akiwa hoi na kuwekwa katika buti ya gari ndogo kwa ajili ya kwenda mafichoni kuteketezwa kwa moto kabla ya kuokolewa na polisi
Kipigo kikiendelea kutoka kwa wananchi wenye hasira kali wakazi wa Ikonongo Mkwawa
 
Kijana anayedaiwa ni mmiliki wa piki piki iliyoibwa (kushoto)

WATUHUMIWA wawili akiwemo mmoja ambaye ni jambazi alitolewa kwa msahama wa Rais Jakaya Kikwete mwaka jana Mohamed Chambogo mkazi wa Ikonongo katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba pikipiki mpya na kusambaratisha na kuiuza kuipima katika mzani na kuiuza kama vyuma chakavu kwa kiasi cha shilingi 20,000 pekee.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotaja majina yao vijana hao ambao walikuwa wakimwadhibu mtuhumiwa huyo walisema kuwa wamelazimika kutaka kumuua kwa kumchoma moto kijana huyo baada ya kuchoshwa na tabia zake za wizi na kuwa hii ni mara ya tatu ananusurika kuuwawa na kuwa awamu ya kwanza alikatwa sehemu zake za siri kwa tuhuma kama hizo.

Wananchi hao walisema kuwa piki piki anayotuhumiwa kuiba ni ya mkazi mwenzao wa eneo hilo na iliibiwa toka mwezi wa tatu mwaka huu na baada ya kutafutwa bila mafanikio jana ndipo walipobahatika kuona mabaki ya piki piki hiyo katika chumba cha mtuhumiwa huyo.

Kwani walisema kuwa mabaki ya piki piki hiyo yalionekana baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo la Ikonongo kata ya Mkwawa kuibiwa mahindi yake kama debe moja hivi na katika msako wa kusaka mahindi hayo ndipo waliposhuhudia mabaki ya piki piki hiyo ambayo chesesi namba yake ilionyesha ni ile ambayo ilikuwa imeibwa kwa mkazi wa eneo hilo.

Hivyo walisema baada ya hapo msako mkali ulianza kwa wanakijiji wote na kufanikiwa kumkamata kijana huyo muda wa saa 1 usiku wakati akirejea kutoka mafichoni akiwa na mali nyingine zinazodhaniwa kwa ni za wizi na ndipo wananchi walipoanza kumpa kichapo na kutaka kumchoma moto kabla ya jeshi la polisi kufika kumuokoa.

Diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thobias Kikula akielezea tukio hilo alisema kuwa katika kata hiyo kumekuwepo na matukio mbali mbali ya uharifu na kuwa tayari mkakati wa pamoja wa kupambana na waharifu hao umewekwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kuwa jeshi lake bado linachunguza zaidi mtandao huo wa uharifu mkoani hapa na kuwapongeza wananchi hao kwa kukamata salama bila kuua watuhumiwa hao wawili.



Source:http://www.francisgodwin.blogspot.com/

Urais 2015 wavuruga chaguzi za CCM

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



MILLIONFORTUNENI UCHAGUZI WA UVCCM, UWT, KILA KAMBI INAJIPANGA KUHAKIKISHA INAWEKA MTU WAKE, SHIGELLA ANASEMA WANAJUA MPANGO HUO

MBIO za kuwania nafasi za uongozi wa juu wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi (CCM), imeshika kasi huku taarifa zikionyesha kwamba kambi zinazowania urais wa 2015 ndani ya chama hicho, kila moja inajipanga kuhakikisha inaweka watu wake.
Wakati katika Umoja wa Wanawake (UWT) hadi jana mchuano ulikuwa ukionyesha kuwa mkali kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela hali ni tofauti kwa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM).
Hadi jana katika mbio za kuwania nafasi ndani ya UVCCM, vijana wanne walikuwa wamechukua fomu kuwania nafasi ya uenyekiti na wengine 16 wakiomba nafasi ya makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo ngazi ya taifa huku Katibu Mkuu wa Umoja huo, Martine Shigella akisema wanafahamu mikakati hiyo ya kambi za urais.
Kwa upande wa UWT, Kilango anaonekana kusimama kundi la makada wa CCM wanaojipambanua kupambana na ufisadi, huku Simba akiwa na kundi jingine tofauti na hilo lakini, pia lenye malengo ya urais wa 2015.
Baadhi ya vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM, vilisema mbali ya nafasi hiyo ya juu ya UWT, kinyang’anyiro hicho pia kipo katika nafasi za wenyeviti wa mikoa.
Tayari vita hiyo ya kambi za urais iko pia katika mikoa ambako kila kambi inajipanga kuweka mtu wake, huku katika Mkoa wa Tabora vita ikitarajiwa kuwa kali zaidi kati ya Margareth Sitta na mgombea wa kambi ya watuhumiwa wa ufisadi.

UVCCM
Kwa upande wa umoja huo wa vijana, kambi hizo zimekuwa zikiumana kuhakikisha kila moja inaweka mtu wake katika nafasi ya uenyekiti, makamu na ujumbe wa Baraza Kuu.
Hadi jana waliokuwa wakiwania nafasi za uenyekiti wa UVCCM Taifa ambao tayari walikuwa wamerejesha fomu ni Thabit Jecha Kombo, Sadifa Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Paul Makonda, Ally Salum Hapi na Agustino Matefu. Makonda alirejesha jana na kuzungumza na waandishi akiahidi kupambana na mafisadi.
Wanaowania nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec), kupitia UVCCM ni Theresia Mtewele, Halima Bulembo, Olivia Sanare, Ahmed Nyangani, Santo Tena, Vaileth Sambilwa, Faidha Salim na Augustino Samwiya.
Katika nafasi za Ujumbe wa Baraza Kuu la Taifa ni, David Mwakiposa, Mteweke Bulembo na Ester Mambali.
UVCCM ni ngome muhimu kimkakati kutokana na kuwa na vijana wengi wanaoweza kufanikisha ajenda mbalimbali ndani na nje ya vikao vya chama na jumuiya.
Uchaguzi huo wa UVCCM unafanyika wakati, kiti cha mwenyekiti kikiwa wazi tangu mwaka 2010 baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake, Yusuf Hamad Masauni kuong’olewa akituhumiwa kudanganya umri na tangu wakati huo nafasi yake ilikuwa ikishikiliwa na Makamu wake, Beno Malisa.
Taarifa ya Sekretarieti ya chama hicho iliyowasilishwa katika kikao cha NEC mjini Dodoma mapema mwaka huu ilieleza kuwa makundi ya urais 2015 ndiyo yanayosababisha mpasuko ndani ya chama hicho.
Shigella: Tunajua
Akizungumzia mikakati hiyo ya vigogo wanaotaka urais kumwaga fedha ili kujiweka mazingira mazuri ya kuwa na watu wao ndani ya UVCCM, Shigella alisema wanajua mipango hiyo na kuonya kwamba kama kuna mgombea ambaye ametumwa na genge la watu wanaotarajia kuwania urais 2015, ajue anapoteza muda kwa sababu hatapitishwa.
Alisema jumuiya hiyo haijawahi kuwa na kiongozi aliyepandikizwa na mtu yoyote.
Alisema watatumia njia mbalimbali kuwabaini watu wa aina hiyo, hasa kwa kuitumia Kamati ya Usalama na Maadili ya jumuiya hiyo na kuwafanyia usaili wagombea na kuangalia historia zao.
“Kwa hiyo, kama kuna wanaowania nafasi za urais mwaka 2015 ambao wametuma vijana kutafuta nafasi UVCCM wafahamu kuwa hawatafanikiwa kwa kuwa tumejiandaa kukabiliana nao,” alisema Shigela.
Makonda na ufisadi
Kwa upande wake Makonda ambaye jana alikuwa wa mwisho kurejesha fomu kwa wiki iliyoisha jana, aliwaambia waandishi wa habari kuwa tatizo la rushwa na ufisadi kwa baadhi ya watu ndani ya UVCCM ndilo lililomsukuma kuwania nafasi hiyo.
Alisema historia ya UVCCM kutoka Tanu Youth League imejengeka katika misingi ya uadilifu na uzalendo, lakini katika siku za karibuni kumekuwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi ambao wamekuwa wakibomoa misingi hiyo na kujenga ya kwao ya kifisadi.
“Hii ndiyo changamoto ambayo imenifanya nijitose katika  kinyanganyiro hiki, si vizuri kuhama chama kikiwa na matatizo. Njia sahihi ni kutafuta uongozi ili kukabiliana nayo. Tukiwa na viongozi bora tutakuwa na uchungu wa namna ya kutatua matatizo ya vijana, kama uchumi na hata mikakati ya ajira,” alisema.
Alisema wakati rushwa ilitajwa kama adui wa haki katika moja ya ahadi 10 za Mwana-TANU, sasa hivi imekuwa ikitumika kama haki ya kupata uongozi hivyo vijana wanyonge wasiokuwa na fedha za kutoa rushwa kukosa nafasi za kuongoza.
Nape: Tumejipanga
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye alisema hafahamu kama kuna vijana wanaowania nafasi mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia vigogo kwenye mbio za urais mwaka 2015.
“Ndiyo kwanza unaniambia, sina habari hizo. Katika CCM tunachoangalia ni kwamba wanaowania nafasi hizo ni kutojihusisha na rushwa vinginevyo hawatakuwa na sifa za kuchaguliwa,” alisema Nape.

Source: http://www.mwananchi.co.tz/

August 6, 2012

JUMUIYA YA KIISLAMU DMV WAFUTURISHA NA KUWAOMBEA DUA WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 Tanzanian Muslim Community Washington Metropolitan (TAMCO) jana Jumapili katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani walifuturisha pamoja na kuwaombea Dua Jamaa wote waliotangulia mbele ya haki. 
Waumini wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu, katika ukumbi wa Hillandale Local Park, New Hampshire Avenue, Silver Spring Maryland nchini Marekani.
Waumuni wakisoma dua pamoja na futari hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Hillandale Local Park New Hampshire Avenue, Silver Spring Maryland. Siku ya Jumapili  Agosti 5, 2012.
 Bwana Omar kutoka State ya Philadelphia alimalizia kwa kuwakumbusha waumini wa Jumaiya, umuhimu wa Dini ya Kiislamu katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.
CHANZO: http://www.globalpublishers.info/

YANGA YATINGA BUNGENI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
yanga watinga bungeni at millionfortune.com
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na wabunge Sylvester Kasulumboyi wa Maswa Mashariki (kulia) na Mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 6, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
wachezaji wa yanga wakiwa na waziri mkuu at millionfortune.com
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Yanga ambao walipeleka Kombe la Michuoano Kagame Bungeni Augost 6, 2012. Kushoto kwake ni Mama Fatuma Karume. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MH. MWANTUMU MAHIZA APOKEA NA KUZINDUA MAGARI YA KISASA YA KUBEBEA WA GONJWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends MILLIONFORTUNE.COM
MILLIONFORTUNE.COM
MILLIONFORTUNE.COM MWANTUMU MAHIZA AZINDUA MAGARI YA WAGONJWA
Mkuu wa mkoa wa pwani Mwantumu Mahiza amezindua  magari mawili ya kubebea wa gonjwa katika hospitali ya Tumbi mkoani pwani magari hayo yame tolewa na serekali ya korea kupitia Rotary intenational club ya tanzania magari hayo yana thamani ya shilngi milioni miambili thelathini za kitanzania kulia ni Jinyong Kim kutoka shirika la kimaendeleo la korea (koika) aliye kushoto ni mwakilshi wa rotary club tanzania bwana  Bill bali  nyuma yao ni mganga mkuuwa hosipitali ya tumbi Dr Petar datani  na aliye nyosha mkono ni mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu kibaha Dr Cyprian mpemba  hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyikia katika hospitali ya tumbi kibaha picha na chris mfinanga

TANZANIA VS MALAWI MMH!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

BREAKING NUUUZ: ASKARI POLISI ALIYEWAANIKA WENZAKE AJINYONGA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Na millionfortune.com
Photo: BREAKING NEWS          BREAKING NEWS. YULE Askari jasiri Donald Julius Mathew mwenye namba za polisi F 3276 aliyejitokeza hazarani na kuwaataja askari wenzake wa mkoani hapa akiwashutumu kwa mambo mbali mbali ya kiwemo ya kushirlikiana na waharifu.  Leo saa 11 Alfajiri mwili wake ulikutwa ukining'inia juu ya mti uliopo jirani na daraja la Shani katikati ya mji wa Morogoro akidaiwa kujinyonga.kabla ya kufika uamuzi huo baadhi ya wananchi wa mkoani hapa jana mchana walimshuhdia Afande huyo ambaye ni maarufu kwa jina la Dunga akilanda landa kwenye mtaa ya mji wa Morogoro huku akionekana kama mtu aliyechnganyikiwa.  Picha zaidi na habari ya tukio hilo tembelea mtandao wa 'www.globalpublisherstz.com' baada ya muda mfupi ujao
YULE Askari jasiri Donald Julius Mathew mwenye namba za polisi F 3276 aliyejitokeza hazarani na kuwaataja askari wenzake wa mkoani hapa akiwashutumu kwa mambo mbali mbali ya kiwemo ya kushirlikiana na waharifu.
Leo saa 11 Alfajiri mwili wake ulikutwa ukining'inia juu ya mti uliopo jirani na daraja la Shani katikati ya mji wa Morogoro akidaiwa kujinyonga.kabla ya kufika uamuzi huo baadhi ya wananchi wa mkoani hapa jana mchana walimshuhdia Afande huyo ambaye ni maarufu kwa jina la Dunga akilanda landa kwenye mtaa ya mji wa Morogoro huku akionekana kama mtu aliyechnganyikiwa.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA EBOLA, KARAGWE, TANZANIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Na millionfortune.com

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA

 Utangulizi

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu tetesi zilizokuwa zimeenea hapa nchini kutoka kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuhusu kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola,wilayani Karagwe mkoa wa  Kagera.

Mnamo tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa Jamii ilipokea taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa mgonjwa aliyekuwa anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, katika hospitali ya  Wilaya ya Nyakahanga. 

Aidha,taarifa hiyo ilibainisha kuwa mgonjwa huyo alikuwa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (6|)  kutoka katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali, kulegea, kutokwa damu puani, kutapika damu,  na kukojoa damu.

Maelezo kutoka kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto huyu alianza kuugua kuanzia tarehe 30 Agosti 2012, ambapo alipatiwa dawa ya Septrin baada ya hospitali binafsi kuonyesha kuwa ana  ugonjwa wa“Typhoid”.

Uchunguzi wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto huyu  alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary Tract Infection).Vile vile alifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na Vipimo vya malaria, Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo  kwa magonjwa haya. Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka mgonjwa na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom room) kwa ajili ya uangalizi zaidi. 

Aidha mnamo tarehe 4 Agosti 2012, timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera imeweza kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina pamoja na kuchukua sampuli za damu kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara ya Taifa ya uchunguzi wa magonjwa na Maabara za nje ya nchi, ili kubaini kama ameathirika na ugonjwa wa Ebola. 

Timu hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa hali ya mgonjwa huyu kwa sasa imeimarika ikiwa pamoja na kutokuwa na homa, kutapika na kukojoa damu kumekoma pia, uchunguzi uliofanywa kwa mama wa mtoto umeonyesha kuwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.Vile vile hakuna taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia hiyo au kwenye maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Kufuatia taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;

• Imepeleka timu ya wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani na mkoa  kwa lengo la kwenda kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo. 
• Imetoa elimu ya Afya kuhusu njia za kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola  pamoja na dalili za ugonjwa huu, kwa wananchi na watumishi wa afya katika hospitali ya Nyakahanga
• Kupeleka vifaa kinga katika hospitali ya Nyakahanga pamoja na maeneo ya mipakani
• Kutoa matangazo kwa jamii kwa kutumia vipaaza sauti na kupitia  radioni (Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu.  Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.

Hitimisho

Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa nchini.Aidha, Wizara ya Afya imejiaanda kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea hapa nchini.

Kwa sasa timu za wataalum  zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha, kutoa elimu juu ya ugonjwa huu kwa wataalamu na kwa wananchi na vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za mipakani.

Wizara inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwenye kituo chochote cha kutolea huduma za afya, mara wanapoona dalili za ugonjwa huu.

Imetolewa na:
 kitengo cha Mawasiliano 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Tarehe 6 Agosti, 2012.

SBL Moshi wamuaga Richard Wells

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Na millionfortune.com
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells wakati wa tafrija maalum ya kumuaga Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (wapili kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda  wakati wa tafrija maalum ya kumuaga Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
Mama Tundu Pinda akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL aliyemaliza muda wake, Richard Wells wakati wa tafrija ya kumuaga iliyofanyika kiwanda cha SBL mjini Moshio hivi karibuni.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi mpya wa SBL, Steven Gannon
Richard Wells (kushoto) akiwa akitika vazi la jadi la jamii ya Wamasaa pamoja na Kisu jamii ya sime alilokabidhiwa na Wafanyakazi wa SBL mjini Moshi wakati walipomuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake na kumkaribisha Mkurugenzi Mpya Steven Gannon.
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Bia Serengeti Mjini Moshi wakipiga picha na viongozi wao.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dr. Msengi
Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda akitunzwa na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela kwa kutoa burudani ya aina yake wakati wa tafrija hiyo ya kumuga Richard Wells.
Vijana wa Kalunde Band wakiwa kazini kutoa burudani
Hapa kazi tu.....Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapundana Mkurugenzi wa Masoko Epraim Mafuru wakiimba wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga Richard Wells.
Richard Wells akicheza mziki na Wafanyakazi wa Kiwanda cha SBL mjini Moshi wakati wa tafrija ya kumuaga.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa SBL, Steven Gannon akisakata rumba na wafanyakazi wa SBL Kiwanda cha Moshi.
Wafanyakazi wakiwa wanaendelea na vitu vya hapa na pale wakati wa tafrija hiyo ya mkumuga Mkurugenzi Mtendaji aliyemaliza muda wake Richard Wells mjini Moshi.

Jaji Bomani azungumza na wajumbe wa tume ya Katiba

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Na millionfortune.com
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Kwanza Mzalendo Jaji Mark Bomani akibadilishana uzoefu na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ofisi ya Tume jijini Dar es Salaam jana (Jumamosi, Agosti 3, 2012). Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim.
Baadhi ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakifuatilia maelezo ya Jaji Mark Bomani aliyekutana nao kwa lengo la kubalishana uzoefu kuhusu Katiba. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana. Picha na habari by mrokin blog

August 4, 2012

HII KALI ZAIDI, DUUH!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
KAMA NI KUTAFUTA HELA MMH...KWAKWLEI HIYO NI KALI!

NEW! NEW!: MATOKEO YA UALIMU NA UFUNDI 2012

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
 
MATOKEO YA UALIMU NA UFUNDI - 2012

DSEE
DTE
GATCE
GATSCCE

JE WAJUA KUHUSU CHRISTIANO RONALDO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Je, Wajua?

   1.
Ronaldo aliitwa jina hilo la Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan, ambaye alikuwa  akipendwa sana na baba wa Ronaldo?
   
2.
Mwigizaji kipenzi wa Cristiano Ronaldo ni nani?
   
3. Wakati Cristiano Ronaldo alikuwa mtoto, aliwahi kumpiga mwalimu wake na kiti kwa sababu alimtania kwa  lafudhi yake ya  Madeiran
?

KUJUA  HAYO NA MENGINE MENGI BOFYA HAPA KUPATA UHONDO KATIKA MILLIONFORTUNE.COM

DONDOO ZA MICHEZO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 

Keita aondoka Barcelona Ahamia klabu ya Dalian Aerbin ya China












Uruguay yaaga olympic

Nyota na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez amewashutumu mashabikii wa Uingereza kwa kuizomea timu yake wakati wimbo wa Taifa lake ukitumbuizwa.Uruguay ilishindwa dhidi ya Uingereza katika mechi kwenye uwanja wa Millennium kwa 1-. Katika michuano mingine Misri ilijiunga na Brazil katika robo fainali na itachuana na Japan iliyoichapa Belarus 3-1

 


Inter yapata wamiliki wa bara Asia
 
Klabu ya Uitaliano Inter Milan inasema kua kundi la wawekezaji kutoka Uchina limejitokeza kua wawekezaji wa pili kwa ukubwa wa kumiliki hisa za klabu hiyo. Wameahidi kujenga uwanja mpya.Klabu hio imetangaza kua Kamchi Li, Kenneth Huang na Fabrizio Rindi wote watakua wakurugenzi kwenye bodi kutokana na uwekezaji huu.


Arsenal kusajili wawili kwa mpigo

Sahin na Cazorla watazamiwa wiki hii. Arsenal inajitahidi kukamilisha utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa kudumu na mchezaji Santi Cazorla kutoka klabu ya Malaga pamoja na mcheza kiungo mwenzake Nuri Sahin anayeingia kwa makubalino ya mkopo kutoka klabu ya Real Madrid.

Ligi Kuu bado haijapata mdhamini

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
WAKATI Ligi Kuu ya Tanzania (TPL) imepangwa kuanza Septemba Mosi ikiwa chini ya Kampuni, mpaka sasa bado hajapatikana mdhamini wa Ligi hiyo ya msimu wa 2012/2013.

Hata hivyo tayari mazungumzo yanaendelea na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom pamoja na kituo cha televisheni cha Super Sports cha Afrika Kusini.

Mmoja wa viongozi waliofanikisha mchakato wa Ligi kuendeshwa kwa kampuni aliiambia Mwananchi kuwa juzi viongozi wa klabu zote 14 za Ligi Kuu walikuwa na kikao kwenye hoteli ya JB Belmonte na kupeana taarifa mbali mbali kuhusiana na mchakato unavyoendelea.

"Mkataba wa Vodacom na TFF ulikuwa ni mkataba wa siri, hata hivyo umemalizika, tumekaa nao kuangalia jinsi ya kuongeza fedha katika mkataba wao na kama tutakubaliana nao basi wataingia mkataba na Kampuni na sio TFF,"alisema kiongozi huyo.

Alisema kuhusu Super Sports ambao awali walisema hawawezi kudhamini ligi ya Tanzania mpaka iondoke mikononi mwa TFF na iendeshwe na chombo huru alisema,"Super Sports pia mazungumzo yanaendelea na tunatarajia itaingia udhamini na kampuni ikishaanza kufanya kazi yake na itaonyesha ligi yetu kama wanavyofanya Kenya."

Tayari Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyokutana siku mbili Jumamosi na Jumapili imeridhia Ligi kuendeshwa na chombo huru na kikao cha juzi pia kilijadili marekebisho madogo madogo ya kisheria ambayo Kamati hiyo ya Utendaji iliomba yafanyike katika muundo huo wa kampuni.

Baadhi ya vipengele ambavyo vipo kwenye muundo huo wa TPL ni kuwa itafahamika kama Ligi Kuu na iwapo atajitokeza mdhamini atanunua jina hilo kwa kipindi fulani na kuweka la kwake ikiwamo kubadili logo ya ligi na atalazimika kutumia logo ya Ligi Kuu kama logo yake mpya na atalazimika kuruhusu angalau kwa asilimia chache jina la Ligi Kuu kuendelea kutumika kwenye ligi.

Pia muundo huo unaonyesha Kampuni ya TPL itaruhusu ligi kudhaminiwa na wadhamini zaidi ya mmoja ambao wanafanya biashara zisizoshindana sokoni na mdhamni yeyote wa Ligi Kuu atazuiwa kuweka logo ya kampuni yake kifuani, ila endapo atatoa fedha kubwa ambayo bodi ya wakurugenzi wa TPL wataridhika kuvaa nembo yake, basi nembo hiyo itawekwa begani na siyo kifuani.

"Kutakuwa na wadhamini wadogo wadogo ambao watauziwa haki ya kutumia logo ya Ligi Kuu kwenye promosheni zao na TPL itawajibika kusaka mdau wa matangazo ya televisheni ili kuweza kupata fedha ya udhamini, nia ni kuboresha mazingira ya udhamini wa Ligi Kuu na udhamini wa klabu,"alisema kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina kwa vile si msemaji wa suala hilo.

Alisema kwa kushirikiana na viongozi wa klabu, meneja masoko wa TPL atakuwa na wajibu wa kusaidia klabu kupata udhamini pia afisa mipango na uendeshaji wa Ligi atafanya kazi chini ya mratibu wa mashindano na atashughulika na klabu kuhakikisha viwanja vina viwango, mechi zinaanza kwa wakati, taratibu zote kabla ya kuanza kwa mechi zinafuatwa na haki za wadhamini wa Ligi Kuu zinalindwa.

Pia mratibu wa mashindano amependekezwa atoke nje ya nchi na atashughulika na mambo yote ya kiufundi kuanzia Usajili, Upangaji wa ratiba, utengenezaji wa kanuni za ligi, mafunzo kwa makocha, waamuzi, mameneja, mweka hazina pia atatoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TPL.

Muundo huo pia umependekeza meneja mawasiliano TPL atafanya kazi kama ofisa habari na meneja mawasiliano wa TPL, pia atatunza rekodi na taarifa zote zitakazohitajika kwa wana habari na pia ataendesha tovuti ya TPL kwa kushirikiana na kampuni itakayoteuliwa kuendesha tovuti ya TPL sambamba na uandaaji wa vipindi vya TV vya TPL kwa kushirikiana na kituo cha televisheni kitakachokuwa na haki za matangazo ya TV.
SOURCE: MWANASPOTI

Clinton:"Khartoum na Juba pataneni"

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

JUBA KHATOOM PATANENI, WAZIRI CLINTON WA MAREKANI AASA

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton amezitaka Sudan na Sudan Kusini kumaliza uhasama baina yao. Akizungumza mjini Juba amesema uhasama ambayo ulizifanya nchi hizo mbili zikaribie vita hazifai kwa nchi ambazo ni jirani.
Bi Clinton ndiye afisa wa kwanza wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kuzuru nchi hiyo tangu ijipatie uhuru Julai mwaka jana.
Makataa iliyowekwa na Umoja wa Mataifa ya kutaka nchi hizo mbili kumalizi tofauti zao kuhusu malipo ya upitishaji wa mafuta ilikamilika jana.
Sudan Kusini ndio nchi ya pili ambayo Bi Clinton anazuru katika ziara yake ya mataifa saba ya bara Afrika.
Waziri huyo aliwasili Juba majira ya alasiri akipitia Senegal akitokea ,Uganda.
"Ijapo Sudan na Sudan Kusini sasa ni nchi tofauti lakini maendeleo yao yanategemea uhusiano kati yao," alisema baada ya kukutana na Rais Salva Kiir was Sudan Kusini.
"Ni jambo la dharura kwa nchi hizi mbili, Kaskazini na Kusini, kuendelea kujadiliana ili muafaka kuhusu utata baina yao uweze kupatikana.
"Kila moja ya nchi hizo ni sharti zilegeze misimamo yao iliklupunguza uhasama kati yao"
Matamshi ya Bi Clinton akiwa Senegal yaliolaumu sera za serikali ya China kuhusu sera zake barani afrika matamshi yake yameshutumiwa na vyombo vya serikali ya China.
Katika taarifa yake mjini Dakar Bi Clinton alisema Marekani inazingatia zaidi mfumo wa uhusiao wenye manufaa kulko ule wa kunyonya raslmali.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat