StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

June 20, 2012

RAIS AMTEUA WAKILI WA LULU KUWA JAJI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
RAIS Jakaya Kikwete amemwapisha kuwa Jaji wakili wa kujitegemea, Joaquine De-Mello ambaye alikuwa akimtetea msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu)  anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba. Wakili huyo, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King ya mwaka 2012 na ambaye alikuwa pia alikuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ni miongoni mwa majaji 10 walioapishwa jana na Rais Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam. De-Mello ni miongoni mwa mawakili wanne waliojitokeza Aprili mwaka huu kumtetea Lulu katika kesi hiyo ya mauaji inayomtuhumu kumuua usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu. Mawakili wengine wanaomtetea Lulu ambaye umri wake umekuwa na utata ni Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Massawe.

Akizungumza kwenye viwanja vya Ikulu, De-Mello alisema baada ya kuteuliwa kuwa Jaji, sasa atafanya kazi hiyo na moja ya mikakati yake ni kukabiliana na changamoto za wingi wa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Majaji wengine walioapishwa jana na Rais Kikwete ni Francis Mutungi, John Mgeta, Patricia Fikirini, Sam Rumanyika, Salvatory Bongole, Jerald Alex, Mathew Mwaim, Jacob Mwambegele na Latifa Mansook. Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alisema amefurahi kuteuliwa kwa majaji hao na anawafahamu kuwa wote ni wazoefu na watatekeleza kazi zao kikamilifu. “Wote ni wazoefu. Ukiangalia utaona kuwa sita walikuwa wakifanya kazi mahakamani (Mahakama Kuu na Rufani), wawili mawakili wa kujitegemea na wawili pia mawakili wa Serikali,” alisema Jaji Othman.
Alisema majaji hao wote kabla ya kupangiwa kazi rasmi itabidi waanze kufanya kazi ya kukabiliana na kesi zaidi ya 2,200 zilizopo katika Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi.

Uteuzi wa majaji hao 10, alisema unaifanya Mahakama Kuu sasa kuwa nao 69 tofauti na wale 16 wanaounda Mahakama ya Rufani. Othman alisema pamoja na uteuzi huo wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kulundikana kwa kesi nyingi kuliko uwezo wao.
“Walioteuliwa watasaidia lakini ukweli ni kwamba bado tunakabiliwa na upungufu wa majaji. Kesi ni nyingi,” alisema Othman. Hakuweza kueleza mara moja idadi kamili ya majaji inayotakiwa ili kukidhi mahitaji lakini akasema kuwa Serikali imeliona hilo na imekuwa ikilifanyia kazi hatua kwa hatua.

Licha ya upungufu wa majaji, Jaji Othman alisema wanakabiliwa na tatizo la kutumia teknolojia ya zamani ya kusikiliza na kuandika tofauti na maendeleo ya sasa ambayo yanahitaji kurekodi.
“Mfumo huu wa kutumia teknolojia ya kisasa pia ungeweza kuharakisha kesi,” alisema Jaji Othman lakini akasema Kitengo cha Biashara tayari kimeanza kuifanyia kazi teknolojia ya kisasa. Kwa kutumia teknolojia hiyo, alisema mtu anaweza kutumia simu yake ya mkononi kujua siku ya kesi yake na hata kuperuzi kwenye mtandao kupata hukumu pamoja na mwenendo wa kesi yake.

Alisema wanatarajia kwenda hatua kwa hatua ili kuhakikisha teknolojia hiyo ya kurahisisha kazi za mahakama inaenea idara zote za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Majaji wengine wapya nao walisema kwenye mahojiano na waandishi wa habari kwamba moja ya changamoto ni kufanya kazi katika mazingira magumu na wingi wa kesi zilizolundikana katika mahakama hiyo.
Jaji Mutungi alisema yeye anaamini kiu kubwa ya Watanzania ni kupatiwa haki na kwamba haki hiyo inapocheleweshwa pia ni tatizo jingine. Ili kuhakikisha anawatekelezea Watanzania haki zao, Mutungi alisema atajitahidi kufanya kazi kwa bidii na kumaliza kesi nyingi kwa haraka.

Kwa upande wake, Jaji Mgeta alisema pamoja na wingi wa kesi kazi kubwa wanayopaswa kuifanya ni kuwa waadilifu na watenda haki. Alikiri kwamba Tanzania wako nyuma katika teknolojia ya kuendesha kesi lakini akasema hilo halipaswi kuwa ni jambo ambalo litawafanya warudi nyuma na kutotekeleza wajibu wao kikamilifu.
Chanzo: Mwananchi

MELI YA KISASA ZAIDI NCHINI AZAM SEALINK: INABEBA MAGARI 200, NA ABIRIA 1500, ITAFANYA SAFARI ZA DAR PEMBA ZANZIBAR

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Azam yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.

Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.

Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.

WAZEE YANGA WAPUNGUZWA MAKALI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
KAMATI ya Uchaguzi Klabu ya Yanga imesema inakerwa na tabia ya Baraza la Wazee la Yanga kuingilia kati masuala ya uchaguzi na kulitaka kukaa pembeni na kuipa fursa kamati husika kufanya kazi hiyo.

Sambamba na kauli hiyo, wagombea watatu wa uchaguzi wa klabu hiyo baadaye mwezi ujao, wamewekewa pingamizi, huku pia zoezi la usaili likipelekwa mbele mpaka Juni 22.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, John Mkwawa alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, kamati yake ni huru hivyo haipaswi kuingiliwa na mtu au kikundi chochote.

Mkwawa alisema kamati yake ina mamlaka ya kumchukulia hatua mtu yeyote atakayekwenda kinyume na taratibu za uchaguzi ambazo wao ndiyo wenye jukumu la kusimamia.

Kauli hiyo ya Mkwawa imekuja siku moja baada ya mwanzoni mwa wiki hii baraza hilo ya Yanga kutishia kumfukuza uanachama  Ahmed Falcon.

Falcon alitishiwa kufukuzwa uanachama kufuatia uamuzi wake wa kuiwekea pingamizi katiba ya Yanga pamoja na wagombea wote wa uchaguzi huo.

Katika madai yake, Falcon alisema katiba inayotumika kwenye uchaguzi huo ni batili kwa vile ina upungufu, jambo ambalo lilipingwa na wazee.

Lakini kwa upande wake, Mkwawa aliwataka wale wote waliowawekea pingamizi wagombea kwenye uchaguzi huo kuwasilisha vithibitisho leo Makao Makuu ya Klabu.

Wagombea waliowekewa pingamizi ni pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini, Ally Mayayi na Stanley Kevela.

Aidha, Mkwawa amesema kamati yake imetupilia mbali pingamizi la mwanachama Falcon kwa madai kuwa halina msingi.

Mkwawa alisema madai ya Falcon hayana mashiko na yameshindwa kuwashawishi kukubaliana naye kwa vile katiba itakayotumika kwenye uchaguzi huo inatambulika kisheria.

"Katiba inayotumika ni mwaka 2010, inatambulika kisheria na imepitishwa na Msajili wa Vyama vya Michezo na kukubaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)," alisema Mkwawa.

Ikumbukwe pia kuwa, baraza hilo la wazee Yanga ndilo lililokuwa chemchem ya vuguvugu la mageuzi ya kutaka mabadiliko ya uongozi kwenye klabu hiyo.

Wazee hao walianza kwa kutaka kukabidhiwa timu siku chache kabla ya Yanga kupambana na Simba katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu, ambao Yanga walifungwa mabao 5-0.
Hata hivyo madai yao yalipingwa na uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Llyod Nchunga na baada ya siku chache wakaanzisha shinikizo la kutaka mwenyekiti wao kuachia ngazi.
Katika kutimiza matakwa yao, baraza hilo la wazee liliitisha mkutano wa wanachama uliofanyika Makao Makuu ya Klabu hiyo lakini bila baraka za uongozi na kutangaza kumtimua Nchunga.
Hata hivyo, mapinduzi hayo yalipingwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kabla ya Mwenyekiti Nchunga kukubalia kuachia ngazi baada ya shinikizo la kumtaka kuachia ngazi kukolea.

WARIOBA: RUKSA KUJADILI MUUNGANO, HATA WALE WANAOTAKA UVUNJWE WALETE MAONI YAO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
MWENYEKITI wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao hata kama ni ya kutaka kuvunja Muungano katika mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya.  Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja kipindi ambacho kuna vuguvugu la kutaka Zanzibar ijitenge, linalofanywa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIK), na kusababisha machafuko visiwano humo.

Jana, Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari kutangaza kuanza rasmi kazi kwa tume hiyo tangu ilipozinduliwa rasmi April 13, mwaka huu, aliweka wazi msimamo huo unaoondoa mkanganyiko katika suala hilo.  Kumekuwapo sintofahamu kuhusu msimamo wa Serikali juu ya Muungano, hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza suala hilo kama moja ya tunu za Taifa, ambayo haitakiwi kujadiliwa kwa lengo la kuuvunja. Jaji Warioba alifafanua kwamba, tume hiyo inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kwamba itakusanya maoni yote na kuyaratibu, ili kupata Katiba wanayoitaka wananchi wenyewe.  “Tume inafanya kazi kwa kufuata sheria. Na kwa kuwa klatika mchakato ni lazima tuanze na Katiba ya sasa, kwanza wananchi waseme upungufu wake. Wananchi wako huru kupendekeza, kwa mfano, kuwepo kwa Serikali yaani Bunge na Mahakama, labda wanataka tuwe na Rais dikteta, waseme,” alisema Jaji Warioba na kuongeza: “Kuhusu Muungano, tutayapokea maoni yote. Kama wanataka mambo ya Muungano yapunguzwe, au yaongezwe, Serikali moja au mbili au wanataka tuvunje Muungano, yote tutayapokea. Tusiseme watu wamezuiwa, hakuna aliyezuiwa.”          

Akifafanua kifungu cha tisa cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayotumika katika mchakato huo, Jaji Warioba alisema Katiba haiwezi kuundwa kama hakuna nchi, ndiyo maana, suala la Muungano limewekwa kuwa la msingi.  Kifungu hicho kinazungumzia mambo ya msingi (tunu za taifa), ambayo Tume ya Katiba itayazingatia wakati wa kukusanya maoni ya wananchi.  “Muswada wa kwanza uliyataja hayo mambo ya msingi kama matakatifu, lakini marekebisho yaliyofuatia yalibadilisha na kuweka kuwa mambo ya msingi. Tume inayazingatia kwa sababu huwezi kuunda Katiba kama hakuna nchi.

Katiba tuliyonayo inasema Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano,” alifafanua Jaji Warioba. Kuhusu tume hiyo kufanya kazi Zanzibar kabla Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haijaridhiwa na Baraza la Wawakilishi, Jaji Warioba alisema Katiba ya Zanzibar haisemi hivyo, badala yake inaelekeza kutoa taarifa tu.  “Utaratibu uliopo ni sheria kuwekwa mezani, ndivyo ilivyo. Sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano zinatakiwa ziwekwe mezani, Baraza haliendi kujadili bali linapewa tu taarifa,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:,  “Sheria hii ilitungwa Novemba mwaka jana na Baraza limekutana Januari mwaka huu.

Kwa utaratibu wa kawaida ilitakiwa iwekwe mezani kwenye Baraza mwezi huo, lakini kukawa na marekebisho mwezi Februari, baada ya hapo tukaipeleka. Sisi tume wala hatuna wasiwasi kwa sababu hilo limeshapita.” Kifungu cha 132 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinasema:

 “Hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na kifungu cha 132 (2) kinasema, “ Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.”

Uratibu wa maoni
Kuhusu  uratibu wa maoni ya Katiba, Jaji Warioba alitaja maeneo manne muhimu yaliyopewa uzito katika ukusanyaji wa maoni kuwa ni misingi ya Taifa ambayo ni uhuru, haki, udugu, amani, demokrasia na Serikali kutofungamana na dini yoyote, ingawa wananchi wake wana uhuru wa kuabudu, huku eneo la pili likiwa ni mamlaka ya wananchi.

“Kuna watu wanasema mamlaka ya wananchi hayakufafanuliwa kama vile Serikali, Bunge na Mahakama, tume ingependa kusikia maoni ya wakulima, wafanyakazi, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wanaume, wanawake, wazee, vijana na walemavu,” alisema.   Aliyataja maeneo mengine kuwa ni malengo muhimu na msingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali, kama inavyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya tisa na eneo la Haki za Binadamu na wajibu wa jamii, kama inavyoelezwa katika sehemu ya tatu ya Katiba.

Marupurupu ya Tume/ Utaratibu
Akizungumzia madai kwamba wajumbe wa tume hiyo wanalipwa marupurupu mengi, Jaji Warioba japo hakufafanua mishahara ya wajumbe alisema hizo ni tetesi zisizo na ukweli.

“Nimesikia ‘speculations’ (tetesi) nyingi kuhusu hayo. Lakini, ninyi mtubane kwa kazi tuliyopewa ya kukusanya maoni….Hapa kuna wengine wana mapato ya chini kuliko huko walikokuwa, kwa kuwa tu wanaona umuhimu wa kulitumikia taifa lao… Sijui kila mtu analipwa kiasi gani…,” alisema Jaji Warioba. Akizungumzia utaratibu wa kazi wa tume hiyo, Jaji Warioba alisema kuwa tume hiyo itaanza kazi katika mikoa minane ya Dodoma, Kagera, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Pwani, Shinyanga na Tanga.

Aliongeza kuwa tume hiyo itakuwa na nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi, ikiwa ni pamoja nakala 500,000 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano, nakala 10,000 za Katiba ya Zanzibar na nakala 500,000 za Sheria ya Katiba ya mwaka 2012.  Alisema baada ya kukusanya maoni hayo, Tume itakutana na mabaraza ya Katiba na mwishowe rasimu ya Katiba itafikishwa kwenye Bunge Maalum.  Aliwataka waandishi wa habari kuwaelimisha wananchi ili waone umuhimu wa kushiriki katika mchakato huo.

Vurugu za JUMIK
Hivi karibuni visiwa vya Zanzibar na viunga vyake vilikumbwa na vurugu kubwa baada ya kundi la Uamsho kufanya vurugu na kutaka visiwa hivyo vijitenge kuwa dola huru. Hata hivyo, vurugu hizo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi, lakini juzi zililipuka upya na polisi kulazima tena kutumia nguvu kuzidhibiti.

MAGAZETINI LEO:UWOYA KALA RAMBIRAMBI ZA KANUMBA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
KUNA habari kwamba mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, ‘picha haziendi’ na mwigizaji wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya kutokana na mama huyo kudai fedha za rambirambi kwa Uwoya alizodai amezila.
Hivi karibuni Uwoya na wenzake Patchou Mwamba na Juma Chikoka ‘Chopa’ walikuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kumalizia msiba wa swahiba wao huyo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Chopa aliyekuwa miongoni mwa walikuwa nchini humo, alisema kuwa baada ya kurejea nchini, mama Kanumba aliwataka waende nyumbani kwake na fedha za rambirambi walizopewa kama pole wakiwa Kongo, jambo lililoshangaza sana.
“Sisi tulikwenda Kongo kwa heshima ya marehemu Kanumba na pia kuendeleza uhusiano mzuri aliokuwa ameanza kuutengeneza ndiyo maana wengine wamejilipia nauli. Kutudai rambirambi kumetushangaza sana, anategemea hizo fedha zitatoka wapi?” alisema Chopa kwa mtindo wa kuhoji.
Kwa upande wa Uwoya, alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, alikiri kuwa ni kweli amesikia kuwa mama Kanumba anadai rambirambi za msiba wa mwanaye kwa wasanii waliokuwa nchini Kongo akiwemo yeye na kueleza masikitiko yake.
“Sasa mama Kanumba anategemea hizo fedha tunazitoa wapi? Hajui jinsi tulivyopata shida ya usafiri wa kwenda na kurudi, wengine tumelazimika kujigharamia wenyewe nauli, hii yote ikiwa ni kumuenzi mwenzetu, sasa yeye anadai fedha za kutoka wapi?” alihoji Uwoya.
Baada ya kusikia kutoka upande mmoja wa wasanii waliokwenda Kongo, Risasi Mchanganyiko lilitenda haki kwa kutafuta mzani wa madai hayo kutoka upande wa pili, likamvutia waya Mama Kanumba ambaye alitoa ushirikiano.
Mama Kanumba alisema, ameshangazwa sana kusikia kuwa Uwoya na wenzake wamesafiri kwenda Kongo kwa ajili ya kumalizia msiba wa mwanaye bila kumpa taarifa akahoji; Nani amewapa ruksa ya kufanya hivyo?
“Nimesikia wamekwenda Kongo kumalizia msiba wa mwanangu lakini mpaka sasa sijajua mwanafamilia gani aliyewapa ruksa ya wao kwenda huko. Pia sijapewa chochote walichorudi nacho kutoka huko.
“Uwoya na wenzake walete pesa za rambirambi za mwanangu walizopewa Kongo vinginevyo hatutaelewana,” alisema Mama Kanumba.
UHUSIANO WA UWOYA, PATCHOU, CHOPA NA KANUMBA
Kwa namna moja au nyingine, Uwoya na Patchou Mwamba walisaidiwa sana kuingia katika sanaa ya uigizaji na marehemu Kanumba.
Uwoya alitokea kwenye tasnia ya urembo na Patchou akiwa ni mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, kazi anayoifanya hadi sasa.
Kwa upande wa Chopa, alianza kujuana na Kanumba tangu wakiwa pamoja katika Kundi la Kaole Sanaa. Ukaribu wao na marehemu ndiyo uliowafanya wasafiri hadi nchini Kongo kumalizia msiba wa swahiba wao huyo.Chanzo:www.globalpublishers.info

MWILI WA WILLY EDWARD OGUNDE KUAGWA LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
MWILI wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, unatarajiwa kuagwa leo kuanzia Saa 4:00 asubuhi kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Willy alifariki ghafla usiku wa kuamkia Jumapili mjini Morogoro, baada ya kuanguka kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na maradhi ya moyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia ya mzee Edward Ogunde, baada ya mwili huo kuagwa, utasafirishwa kwenda Mugumu, Serengeti, Mara kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika Juni 23, mwaka huu.
“Msiba upo nyumbani kwa kaka yake mkubwa, ndugu Denis Ongiri eneo la Mburahati-Msikitini jijini Dar es Salaam. Mazishi yatafanyika nyumbani kwao kitongoji cha Morotonga, Mugumu, Serengeti,” ilisema Taarifa hiyo.

MNYIKA ATOLEWA BUNGENI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika ametolewa katika ukumbi wa Bunge la Tanzania mapema jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
 Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho.
Mh. John Mnyika akichangia bungeni

G20 leaders call for Europe to fix finance woes

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
European leaders at the G20 summit are struggling to reassure the world that they are on the path to solving their continent's relentless economic crisis, defending the pace of their response even as market pressures pushed Spain closer to needing a bailout that would strain the world's ability to pay.
Less than 24 hours after an election that eased fears of a Greek exit from the shared euro currency, the interest rate that Spain pays on its debt surged above the 7-percent level that had forced Greece, Portugal and Ireland to seek international help.
The prospect of a bailout for Spain's €1.1 trillion economy immediately eclipsed the good feeling at the G20 from the election, and it dwarfed the host country Mexico's expressions of confidence that the meeting of the world's largest economies would lead to more than $430 billion in concrete commitment for the International Monetary Fund as insurance against future bailouts.
The Spanish delegation to the G20 bemoaned the rise in the country's borrowing costs and said the market reaction didn't correspond to the reality of Spain's economic strength.
"We in the government are convinced that the current situation of punishment in the markets, what we're suffering from today, doesn't correspond with the efforts, or the potential, of the Spanish economy," Spain's economy minister Luis de Guindos said. "This is something that will have to be recognised in the coming days and weeks."
The day was filled with statements from a variety of world leaders calling for cooperation and for Europe to solve its crisis at a summit that is expected to produce few concrete results.
"Now is the time as we've discussed to make sure all of us join to do what's necessary to stabilise the world financial system, to avoid protectionism, to both grow the economy and create jobs while taking a responsible approach," US President Barack Obama said after meeting with the host, Mexican President Felipe Calderon.
European Commission President Jose Manuel Barroso and European Council President Herman Van Rompuy urged markets to focus on a European summit at the end of the month that they said would help the continent move closer to deeper economic and political integration to match its single currency. The lack of common rules for the countries sharing the euro currency is seen as the primary cause of the current crisis. The EU summit would bring progress on common banking rules for member nations, Barroso and Van Rompuy said, although they cautioned, in sometimes defensive tones, against expectations of short-term results.
"I can assure you that even if we in June will not take definitive decisions, the path, the trajectory is very clear for everybody," Van Rompuy said. "In this case, the pace is less important than the decision we make."
Barroso took a more aggressive tone, declaring that "the crisis originated in North America" with the collapse of real-estate-linked financial products and taking a subtle dig at China and other non-democratic countries at the summit.
"Not all the members of the G20 are democracies, but we are democracies, and we take decisions democratically. Sometimes this means taking more time," he said. "Frankly we are not coming here to receive lessons in terms of democracy or in terms of how to handle the economy, because the European Union has a model that we may be very proud of."

Hosni Mubarak on life support after heart stops

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Egypt's Hosni Mubarak is on life support after his heart stopped as he arrived at a military hospital.
The state news agency MENA said the 84-year-old Mubarak was "clinically dead" when he arrived at the hospital from prison. It said doctors used a defibrillator on him several times.
MENA initially said the efforts were not successful.
But the official said Mubarak was put on life support. He had no further details on his condition. The official spoke on condition of anonymity because he was not authorised to talk to the press.
Mubarak was moved out of prison to a military hospital after the 84-year-old ousted leader suffered a stroke and his condition rapidly deteriorated, officials said.
It adds a new element of uncertainty just as a potentially explosive fight opened over who will succeed him, with both candidates claiming to have won last weekend's presidential election.
The developments add further layers to what is threatening to become a new chapter of unrest and political power struggles in Egypt, 16 months after Mubarak was ousted by a popular uprising demanding democracy.
The campaign of Mubarak's former prime minister, Ahmed Shafiq, said Tuesday he has won Egypt's presidential election, countering the Muslim Brotherhood's claim of victory for its candidate, Mohammed Morsi.
The election commission is to announce the official final results on Thursday and no matter who it names as victor, his rival is likely to reject the result as a fraud. If Shafiq is declared winner in particular, it could spark an explosive backlash from the Brotherhood.
The Brotherhood, Egypt's most powerful political group, is already escalating its challenge against the ruling military over the generals' move this week to give themselves overwhelming authority over the next president. Some 50,000 protesters, mostly Islamists, massed in Cairo's Tahrir Square on Tuesday evening chanting slogans in support of Morsi and denouncing the generals' power grab.
Since June 2, Mubarak has been serving a life sentence at Cairo's Torah Prison for failing to stop the killing of protesters during the 18-day uprising against his rule last year. The verdict against him has already been a spark for protests - thousands massed in Tahrir when the court acquitted him and his sons on separate corruption charges and cleared several top security chiefs on the protester killings.

June 19, 2012

AFRICAN THEME "NYC PARTY FOR JESCA'S BIRTHDAY"

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 mapochopocho
 Picha za pamoja
 Mabinti nao..mh
 Jamani...! ilikuwa raha
 Hapo sasa...
 Na Dj alikuwa wa ukweli
Kwakweli wala sinahaja ya kuongeza lolote jionee mwenyewe walivyofaidi...

DAR LIVE INAKULETEA WANAUME FAMILY SPESHO J'PILI HII

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
USIPANGE KUIKOSA HII...!

JUMA NATURE, ROMA NA MWASITI KUFUNIKA TAMASHA LA AIRTEL SUPA5 MWISHONI MWA WIKI HII MWANZA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mchakato wa kuendelea kuitambulisha huduma ya Airtel Supa5 mikoani utaendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo Airtel itaweka kambi mkoani Mwanza katika viwanja vya wazi vya Furahisha vilivyopo jijini Mwanza.
Akizungumzia tamasha hilo la kuitambulisha SUPA5 mkoani Mwanza Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema lengo la kuunganisha utambulisho huu burudani ni kuwavutia vijana na wateja wengi kuhudhuria na kujifunza faida lukuki za SUPA5 ili waitumie zaidi.
Tamasha linafanyika kwa siku mbili mfululizo ambapo siku ya Jumamosi tunatoa fulsa kwa wasanii chipukizi kujitokeza kwa wingi kuonyesha vipaji vyao sambamba na kupata huduma ya Airtel SUPA5.
Jumapili itakuwa uzinduzi kamili ambapo wasanii wakubwa watatoa burudani BURE, akiwemo Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Mwasiti a.k.a SOJA, Roma Mkatoliki a.k.a mzee wa tuzo kibao watatoa burudani kali kwa wateja watakaohuduria tamasha hilo BURE.
Bi Matinde pia amezungumzia lengo la huduma ya dili tano bomba zilizopo kwenye huduma ya SUPA5 kuwa Airtel inatimiza dhamira yake iliyojiwekea ya kufikisha na kupunguza gharama za mawasiliano nchini kote bila kuwasahau vijana na wanafunzi kunufaika kwa kupata internet bure wakati wa usiku, kutuma sms bure na faida nyingine nyingi.
Huduma ya Airtel SUPA5 ilizinduliwa rasmi siku za karibuni jijini Dar es Salaam kisha kufuatiliwa na kufanyika kwa matamasha ya burudani ya BURE katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Arusha huku mwishoni mwa wiki hii itakuwa zamu ya wakazi wote wa Mwanza.
Wasanii mahiri waliokwishapamba majukwaa ya Airtel SUPA5 hadi sasa kwa mkoa wa Dar es salaam ni Fid Q, Mwasiti, Godzilla, pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madee, Tundaman, Richard na Dogo Janja kwa mkoa wa IRINGA ni Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Roma Mkatoliki, pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madee, Tundaman na Richard. Mkoa wa Morogoro na Dodoma ni kundi mahiri la Wanaume Family likiongozwa na Chegge na Temba na kukamilisha ladha ya zaidi kwa kuwepo kwa Bendi Maarufu jijini ya Mashujaa ikiongozwa na kingunge Charles Baba na wasanii wengine.

MKOKO MPYA WA DIAMOND PLATINUMZ

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mwanamuziki anayetikisa ktk anaga za muziki wa kizazi kipya Diamond Platinum akiwa ktk pozi tofauti na gari lake jipya aina ya Prado
 Gari hilo kwa mwonekano wa pembeni milango ikiwa wazi
 Mwonekano wa ndani wa gari la diamond platinum

WAREMBO MISS DAR INTERCOLLEGE KUSUGUA KISIGINO CHA TWANGA, CLUB BILICANAS KESHO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 Jumatano ya kesho wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo msanii wa bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "Twanga Pepeta' kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila Jumatano katika klabu hiyo.
Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao.
"Warembo wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga Pepeta hutumbuiza kila Jumatano kupitia usiku wa Mwafrika, hivyo tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashuhudia kabla ya kuja tena Ijumaa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,"Alisema.
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaoshiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania,” alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT) ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Dinaismail (zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKISHO LA BASKETBALL NCHINI TANZANIA (TBF)

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




Rais Jakaya Kikwete akipokea jezi ya timu ya Mpira wa Kikapu inayocheza ligi ya NBA ya Marekani New York Knicks toka kwa Rais wa Shirikisho la  Basketball (TBF), Bw Mussa Mziya na Makamu wake Bw Phares Magessa walipomtembelea leo  Ikulu Jijini Dar es Salaam  na kumueleza mipango ya chama hicho katika kuinua vipaji na viwango vya mchezo.



Rais Jakaya Kikwete akipokea jezi ya timu ya Mpira wa Kikapu inayocheza ligi ya NBA ya Marekani New York Knicks toka kwa Rais wa Shirikisho la  Basketball (TBF), Bw Mussa Mziya na Makamu wake, Bw Phares Magessa walipomtembelea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumueleza mipango ya chama hicho katika kuinua vipaji na viwango vya mchezo.


Rais Jakaya Kikwete akiongea na Rais wa Shirikisho la Basketball, (TBF) Bw Mussa Mziya na Makamu wake Bw Phares Magessa walipomtembelea leo  Ikulu Jijini Dar es Salaam  na kumueleza mipango ya chama hicho katika kuinua vipaji na viwango vya mchezo.
(Picha na IKULU)

 

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE AAPISHA MWENYEKITI MPYA NA MAKAMISHNA WA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
MWENYE KITI MPYA WA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI AKILA KIAPO MBELE YA MH. RAIS KIKWETE
MOJA YA MAKAMISHNA WAPYA, NDUGU MARY CRESENT AKILA KIAPO
MWENYEKITI MPYA NA MAKAMISHNA WAPYA KATIKA PICHA MOJA NA MH. RAIS KIKWETE BAADA YA KUAPISHWA RASMI.

KILIMANJARO, Ajali yaua 5, yajeruhi 13

Tweeted this Like this, be the first of your Friends AJALI za barabarani zimeendelea kuutikisa Mkoa wa Kilimanjaro, jana basi dogo la abiria liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo na kujeruhi 13.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhan Ng’azi, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 1:00  usiku wakati basi hilo likitokea Kijiji cha Ng’uni kwenda Bomang’ombe, kupitia Kware wilayani Hai.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Mbosho, Kata ya Masama, baada ya dereva wa basi hilo dogo aina ya Toyota Hiace namba T179  AAX ambaye hajafahamika, kushindwa kudhibiti gari hilo.

Ng’azi alisema waliokufa wametambuliwa kuwa ni Elinawenga Leama (90) mkazi wa Isuka, Fred Jackson (23) mkazi wa Masama na Raphael Kimaro(55) mkazi wa Ng’uni.
Wengine waliokufa ni Richard Munuo (55) mkazi wa Kijiji cha Ng’uni na Baraka Ng’oko (45), ambaye ni mkazi wa Arusha.

Waliojeruhiwa na umri wao ukiwa kwenye mabano, ni Oscar Siao (40-45), Alisenda Sirael (50), Leonard Munisi (32), Hussein Abdi (63), Aminadabu Munuo(6) na Richard Arnold (18).

Wengine waliojeruhiwa ni David Joshua (39), Noel Onesmo (25), Marry Witness (44), Walter Tarimo (37), Onisael Anankya (70), Helea Ngunda (60) na Wilinanda Amosi (37).

Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Kibong’oto ,wakati majeruhi walipelekwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu.

Kaimu kamanda huyo alisema ingawa uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea, lakini inaonyesha mwendokasi umechangia kwa kiwango kikubwa.

Wizi fedha kiasi cha Tsh 3.5 billioni za safari za JK kufanyiwa uchunguzi

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe jana alizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma za wizi wa kiasi cha Tsh. 3.5billion zinazodaiwa kupotea/kutumika katika mazingira yasieleweka.
Aidha hivi karibuni, SERIKALI imeanza uchunguzi wenye lengo la kubaini kama maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walifuata taratibu kutoa kutoka Hazina Sh3.5 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya safari za Rais Jakaya Kikwete ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe alisema jana kuwa fedha zinazochunguzwa ni zile zilitolewa kati ya Machi Mosi na Machi 8, mwaka huu kwa ajili ya safari za Rais Kikwete kwenda Geneva, Brazil, Adis Ababa na Arusha.

Wiki iliyopita gazeti moja la kila wiki liliripoti kuwa maofisa watano wa wizara hiyo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa kwa ajili ya safari za rais kutoka benki moja nchini.

Fedha zilizotolewa kutoka Hazina ni Sh 3.5 bilioni wakati zilizokuwa zimepangwa kwa safari hizo ni Sh2 bilioni.Fedha hizo zinadaiwa kutolewa Hazina na maofisa waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali, katika wizara hiyo.

Waziri Membe alisema wakati tukio hilo likitokea, yeye, naibu wake, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu walikuwa safarini na kwamba nafasi zao zilikuwa zinakaimiwa.
“Waliokuwa wanakaimu wali-process (andaa) fedha za safari pamoja na hazina, na fedha zikapatikana tarehe 8,” alisema Membe na kuongeza kuwa;
“Ofisa Masuhuri hakushirikishwa na uchunguzi wa kamati unaendelea ili kujiridhisha kama taratibu zote za kiutawala zilifuatwa,” alisema.

Alifafanua kwamba tayari walifanya uchunguzi uliohusisha Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa na wakaguzi wawili kutoka wizarani hapo.
“Hakuna tuliyemshuku ama kumuita mwizi kwa sababu hakuna hata fedha iliyoibwa, zote ziliingia kwenye akaunti ya wizara na nyingine zililetwa wizarani,” alisema.
Waziri huyo alisema uchunguzi wa kamati unaoendelea, sasa unalenga kuangalia kama taratibu zilifuatwa na wale waliokuwa wanakaimu.“Uchunguzi wa kamati utakapokamilika na kubainika makosa yalikuwa wapi utawekwa hadharani,” aliahidi.
Utabiri wake Chadema
Akizungumzia taarifa za kuitabiria Chadema ushindi mwaka 2015, Membe aliwatuhumu watu aliowaita maadui wake kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema wameshiriki kumlisha maneno ya kukitabaria ushindi chama hicho kikuu cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Kuna taarifa za mimi kutabiria ushindi Chadema 2015. Naomba niseme kitu kimoja, kama kuna mtu anajua mimi niliwahi kufanya utabiri ajitokeze. Mimi siyo TB Joshua wa Nigeria, mtoto wa marehemu Shehe Yahaya au (jina la kampuni moja ya kimataifa)...ambao wao kila mara ndiyo hufanya utabiri," alisema Membe huku akionekana kuchukizwa na taarifa hizo.

Membe alifafanua kwamba, ni kweli alikutana na ujumbe wa Chadema nyumbani kwake jimbo la Mtama, mkoani Lindi na kufanya nao mazungumzo, lakini hakuwahi kutabiri kwamba chama hicho kikuu cha upinzani kingeweza kushinda mwaka 2015.

"Nikweli nilifanya mazungumzo na Chadema walipokuja jimboni kwangu Mtama. Tena walikuja bahati nzuri walikuta chakula cha mchana tayari, nikawakaribisha vizuri. Wapinzani si maadui, yaani watu walitaka niwafukuze chakula. Najua kuna watu hawakufurahia kuwaalika Chadema kuja kwangu," alisema Membe na kuongeza;

"Ni kweli niliongea nao. Niliongea nao mambo matatu, kwanza niliwapongeza kwa kujipenyeza hadi vijijini. Niliwaambia, ni vema mmetambua umuhimu wa kufika hadi vijijini maana mwaka 2010 mlilalamika kuibiwa kura wakati vijijini mlikuwa hamjafika. Lakini pia, nikawambia ni vema wametambua umuhimu wa kuanza kufanya siasa kwa kujenga hoja na tatu, nikawambia nyie fikeni vijijini sisi kina Membe hatujaanza kutimua vumbi."

Alifafanua kwamba, anaamini watu wa Chadema waliokuwapo katika mkutano huo ambao ni pamoja na Dk Slaa na Lema hawawezi kuzusha taarifa hizo zilizotolewa na kuongeza, "Nimesoma vizuri Political Science, adui wa kisiasa katika chama siku zote yumo ndani ya chama hicho. Kwa hiyo hata hili naamini limetoka kwa baadhi ya maadui ndani ya CCM na kwa Chadema ni maadui wa Chadema."

Kuhusu APRM
Katika hatua nyingine, Membe alisema taarifa ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kujitathmini wa Umoja wa Afrika (APRM), itajadiliwa mwakani nchini Addis Ababa.

Licha ya waziri huyo kukiri kwamba Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000 za ada, alisema hiyo si sababu ya taarifa ya Tanzania kutojadiliwa mwaka huu kama ilivyotarajiwa.

Rais Kikwete alitarajiwa kuwasilisha ripoti ya Tanzania kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU), utakaofanyika Lilongwe, Malawi Julai 10 mwaka huu, lakini haitafanyika hivyo.Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuwa Rais Kikwete amezuiwa kuwasilisha taarifa ya Tanzania kutokana na deni hilo.

“Walitakiwa wajadili taarifa ile halafu walete maswali tujibu ndipo wataandaa taarifa ikajadiliwe,” alisema Membe na kuongeza;

“Watu wa APRM hawajaja, hivyo itajadiliwa katika mkutano wa Addis Ababa mwaka 2013,” alisema.
Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000  deni ambalo ni malimbikizo ya ada ya dola 100,000 kila mwaka, kwa miaka minane mfululilizo tangu mwaka 2005.“Mara kwa mara tumekuwa tukiwakumbusha Hazina kuhusu deni hili na si kwamba ndilo limezuia,” alisema.

Dr. Edward Hosea afungua mkutano Arusha kuhusu changamoto za tatizo la rushwa africa

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Bodi ya ushauri ya masuala ya rushwa Afrika inakutana kwa wiki nzima jijini Arusha hivi karibuni ili kuandaa taarifa ya hali ya rushwa itakayowasilishwa katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao Adis Ababa Ethiopia.

Bodi hiyo pamoja na mambo mengine,itapitia kwa mapana changamoto za rushwa katika nchi wanachama wa AU, sanjari na kutathmini nchi mojamoja katika maeneo yanayolalamikiwa mara kwa mara,ikiwa ni pamoja na rushwa katika uwekezaji,huduma za jamii,na matukio ya rushwa katika chaguzi na siasa ambayo yanatajwa kuwa chanzo cha migogoro barani Afrika.

Dk.Edward Hosea ambae ni mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ,ametoa takwimu za kushtua zinazoonyesha hali halisi ya wizi wa fedha za umma na rushwa katika nchi za Afrika ambazo hutoroshwa kila mwaka na kuhifadhiwa katika nchi zilizoendelea. Amesema kiasi cha Dola bilioni 148 hutoroshwa kutoka Afrika kwenda nchi za ughaibuni kila mwaka kwa sababu ya Rushwa.

Hata hivyo,Mkurugenzi huyo amesema nchi zilizoendelea ambazo mabenki yake yanahifadhi fedha hizo,zinawajibika katika kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa katika nchi zinakoibwa.

Wakati huo huo,Dk.Hosea amesema wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika katika mkutano uliopita,waliteua jiji la Arusha Tanzania kuwa makao makuu ya Bodi ya Ushauri wa masuala ya rushwa barani Afrika na kwamba serikali ya Tanzania tayari imetoa eneo ka ajili ya ujenzi wa makao makuu hayo na kinachosubiriwa ni kuona serikali imetenga kiasi gani  kwa ajili ya ujenzi huo.


Wataalamu mbalimbali wamealikwa kuwasilisha mada katika kikao hicho cha maandalizi,ili kuwawezesha wajumbe wa bodi hiyo kupata uzoefu wa hali na mazingira ya rushwa katika nyanja mbalimbali,huku mtoa mada wa kwanza akiwa ni Mtanzania Jaji Augustin Ramadhani kutoka mahakama ya Afrika ya haki za binadamu.

Zitto aichambua bajeti, aeleza mapungufu yake...HAINA UNAFUU KWA WANACHI WA KAWAIDA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe akiwasilisha bunge bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani Bungeni kwa mwaka wa fedha 2012/2013, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi







ATAJA KASORO ZAKE, ASEMA HAINA UNAFUU KWA WANANCHI WA KAWAIDA
Neville Meena, Dodoma WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe jana aliwasilisha bungeni bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani kwa mwaka wa fedha 2012/2013, huku akibainisha kasoro lukuki katika bajeti ya Serikali ilioyowasilishwa Alhamisi iliyopita.Bajeti ya Zitto ilitanguliwa na hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Rais – Mipango, Christina Mughwai ambaye pia aliweka wazi kile alichokiita udhaifu wa Serikali katika kuitekeleza mipango yake ya kiuchumi, hali ambayo inasababisha umaskini kwa wananchi.

Hotuba zote mbili, ya Zitto na Lissu, zilisema licha ya Serikali kutangaza kwamba bajeti ya 2011/12 ilikuwa ya kupunguza makali ya maisha, hakukuwa na nafuu yoyote kwa wananchi kwani maisha yameendelea kupanda.

Pamoja na kupendekeza njia kadhaa za kupanua wigo wa mapato ya Serikali, wapinzani wametaka kufanywa kwa ukaguzi wa deni la taifa, ili kubaini chanzo cha Serikali kukopa na kuweka wazi jinsi fedha hizo zilivyotumika hadi kufikia Sh22 trilioni.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni katika hotuba yake alisema mapato ya Serikali yanaweza kuongezwa kwa Sh2.885 trilioni, hivyo kupunguza utegemezi wa mikopo ya kibiashara ambayo imekuwa ikiligharimu taifa kiasi kikubwa cha fedha.

Vyanzo vya kodi na kiasi cha fedha kwenye mabano alivyopendekeza ni marekebisho ya kodi za misitu ikiwamo mkaa (Sh130.8 bilioni), Kupunguza misamaha ya kodi, kuzuia ukwepaji kodi na udanganyifu wa biashara ya nje (Sh742.74 bilioni), Mauzo ya hisa za Serikali (Sh415.55 bilioni), Marekebisho ya kodi Sekta ya Madini na asilimia 25 ya Mauzo ya Madini Nje (Sh578.36 bilioni) na Marekebisho ya Kodi na Usimamizi bora wa Mapato Kampuni za Simu (Sh502.26 bilioni).

June 15, 2012

SUVs worth waiting for in 2013

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
es, the auto world is getting crowded with cushy crossovers, but that doesn't mean there aren't any rugged SUVs anymore. Here are the ones we're anticipating in the next few years.

2013 Ford Explorer Sport
When:
Late Summer

We recently drove the new Ford Taurus SHO, a car that is a classic sleeper. It has a 365 hp V-6 under the hood to move the big sedan to 60 mph in a little over 5 seconds, but what's more shocking is that it corners well, too. And if Ford's done its homework, the all-new Ford Explorer Sport will be an SHO-equivalent on the SUV front.

The Explorer Sport gets the same V-6, a significantly beefed up chassis, as well as a stiffened, lowered suspension, bigger brake rotors, and a faster feel to the steering system. All of these tweaks made the Taurus SHO into a much more aggressive machine. Ford is also trying to walk a fine line between all-out performance and reasonable fuel economy with the Sport. Its 16/22 mpg target would be a big improvement on the 12/18 of the Jeep Grand Cherokee SRT8 (which will cost about $10,000 more than the Ford, we think.). Significantly, the Explorer Sport will also do better than the 13/20 of the 5.7-liter, Hemi V-8 Dodge Durango, a vehicle we really like for its great handling, given its mission. If Ford catches up in power and can offer better fuel economy, it's sure to capture a lot of buyers for the Explorer Sport.

Serikali yapunguza kodi ya VAT

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



SERIKALI imepunguza kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutoka asilimia 18 za sasa kuwa asilimia 1O kuanzia Julai1, mwaka huu.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa alilieleza bunge mjini Dodoma wakati akisoma Makadirio na Mapato ya Serikali kwa mwaka 2012/13 jana, kuwa hatua hiyo inalenga kuwianisha kiwango kinachotolewa nchini na kile cha kimataifa.

Watakao nufaika na uamuzi huu ni wote waliokuwa wanalipa kodi hiyo, isipokuwa wale wenye msamaha wa kodi hiyo kwa makubaliano maalum na Serikali.

Wazir ialiwataja watakaonufaika kuwa ni kampuni binafsi, mtu mmoja mmoja, wale walio sajiliwa katika Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Kwa mujibu wa waziri huyo, pia punguzo hilo litayanufaisha mashirika yasiyo kuwa ya kiserikal iisipokuwa yale yanayotoa misaada ya chakula na matibabu kwa watoto, vituo vya watoto yatima na shule.

Vile vile Dk Mgimwa ametangaza kutoa msamaha wa VAT kwa mashine za kutolea stakabadhi (Electronic Fiscal Devices) ili kupunguza bei yake na kuwezesha wafanya biashara wengi kuwa nazo, kuhamasisha matumizi yake hivyo, kuongeza mapato ya Serikali.

Katika eneo hilo, Serikali imeondoa VAT kwa vifaa mbalimbali vya kuhifadhia, kusafirisha na kusambaza gesi asilia ili kuongeza matumizi ya nishati hiyo katika sekta mbalimbali za kiuchumi,  kwenye magari, majumbani na viwandani.

“Lengo ni kutunza misitu, kulinda mazingira na kuhamasisha utengenezeji wa majiko ya gesi hapa nchini,” alisisitiza Dk Mgimwa.

Umeme kipaumbele bajeti ya 2012/13

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Thursday, 14 June 2012 
Claud Mshana
SERIKALI imetenga Sh498.9 bilioni katika bajeti yake ya mwaka ujao wa fedha wa 2012/13, kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini.
Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, uzalishaji wa umeme umepewa kipaumbele kikubwa katika mafanikio ya mpango wa taifa wa maendeleo.Dk Mgimwa aliyasema hayo jana katika hotuba yake kuhusu bajeti ya Serikali katika mwaka wa fedha wa 2012/13.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali pia itaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya nishati ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, mradi utakaogharimu Dola 1.2 milioni za Marekani.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi, fedha hizo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Exim ya China.
Dk Mgimwa alisema pamoja na umeme, miradi mingine ya maendeleo iliyopewa kipaumbele katika bajeti ya mwaka ujao, ni ya  uchukuzi, maji safi na salama.

Hali kadhalika, teknolojia ya habari na mawasiliano, kilimo, maendeleo ya viwanda na utalii.
Alisema ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na hivyo usalama wa chakula, Serikali itahakikisha kuwa inatekeleza kikamilifu, Sera ya Kilimo Kwanza.
Alisema kiasi cha Sh192.2 bilioni kimetengwa ili kugharimia utekelezaji wa Sera ya Kilimo na kwamba fedha hizo zitatumika katika kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kilimo cha kisasa, na kufufua kilimo cha umwagiliaji.

Pia alisema sehemu nyingine ya fedha hizo,itatumika katika kuimarisha soko la mazao kupitia Bodi ya mazao, ambayo tayari imeanza kufanya kazi.
Alibainisha kuwa kwa kushirikiana na sekta binafsi, Serikali itawekeza katika kilimo cha mpunga na miwa katika mabonde makubwa ya Wami, Ruvu, Kilombero na Malagarasi, ili kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao.
“Pia bajeti hii imezingatia kuondoa changamoto mbalimbali zinazozua kuwepo kwa maendeleo, Serikali imedhamiria kuboresha kilimo, kuongeza ajira na kumaliza ukiritimba wa kupata mikopo kwa kuzipatia pesa taasisi  mbalimbali za fedha,” alisema waziri huyo katika hotuba yake.
Taasisi hizo ni pamoja na Benki ya Uwekezaji Nchini (TIB) iliyopewa Sh30 bilioni na Benki ya Maendeleo ya Kilimo iliyopewa Sh40 bilioni.

Dk Mgimwa alisema Serikali pia imetenga  Sh70 bilioni kwa ajili ya matumizi na maendeleo kwa mikoa na wilaya mpya.
 Eneo lingine lililopewa kipaumbele katika bajeti ya mwaka huu, ni kuimarisha miundombinu ya usafiri ikiwemo reli ya kati, usafiri wa anga na wa majini.

Kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama, waziri Mgimwa alisema Sh568.8 bilioni zimetengwa kwa ajili ya huduma za  maji safi na salama mijini na vijijini.

TFF: Yondani atacheza Yanga 100%

Tweeted this Like this, be the first of your Friends



LAMPS COLLIN
UTATA wa usajili wa Kelvin Yondani unaelekea kupata majibu mapema baada ya kuthibitika kuwa ataichezea Yanga msimu ujao.

Mmoja wa wajumbe wa kamati mmojawapo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) aliithibitishia Mwanaspoti jana Jumatatu kuwa Yondani atacheza Yanga msimu ujao baada ya kugundua udanganyifu uliofanyika Simba.

"Hapa tuwe wa kweli. Simba wanasema walimsainisha Yondani Desemba mwaka jana, tunajua kuwa Yondani alikuwa na matatizo na Simba wakati huo angesaini vipi mkataba mpya?" Alihoji mjumbe huyo wa TFF.

Mjumbe huyo alisema Simba wanaonekana kushindwa mapema katika kesi hiyo kwa sababu kama wangekuwa wanamtaka Yondani wangemsainisha kabla hajaingia miezi sita ya mwisho na mkataba wake ungesajiliwa TFF.

"Hivi unadhani Simba wangekuwa wanamtaka Yondani wangesubiri mpaka mkataba wake uishe?" Alihoji.

"Huyu sisi tuna taarifa kuwa alisaini Simba baada ya timu kurejea kutoka Algeria katika Kombe la Shirikisho. Ila walichokifanya ni kurudisha nyuma tarehe ya usajili ili ionekane amesajili Desemba.

"Hata kama amesajili Desemba bado walichelewa kwa sababu wakati huo tayari Yondani alikuwa amebakiza mkataba wa miezi sita, hivyo alikuwa huru kusaini klabu yoyote. "

Mwanaspoti ilipomuuliza Yondani atacheza timu gani msimu ujao alisema: "Kwa mazingira yote hayo ni dhahiri atacheza Yanga kwa asilimia mia."

Familia ya Yondani
Kaka mkubwa wa Kelvin Yondani ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyo, Sunday Patrick ameridhia beki huyo kwenda Jangwani.

Sunday aliiambia Mwanaspoti wiki iliyopita kuwa: "Sisi kama familia kwa moyo mmoja tupo na Yondani katika uamuzi wake, cha msingi yeye amefuata sheria na hana mkataba wowote na Simba ndio maana hata sisi tumempa baraka za kwenda Yanga, pia viongozi wa Simba wanapaswa kufahamu kuwa mchezaji huyu bado ni mdogo na anatafuta maisha hivyo wamuache afanye uamuzi wake."

Kauli ya Yondani
Yondani ambaye awali alidai kusaini Simba, Alhamisi iliyopita aliikana kauli hiyo na kusema amesaini Yanga.
"Nimesaini Yanga, nawatakia kila la kheri Simba."

Yondani amelamba Sh.30 milioni kutoka Yanga na atakuwa akilipwa mshahara wa Sh 800,000 ingawa kuna taarifa kuwa ameongezewa na atakuwa akilipwa Sh milioni moja kwa mwezi huku ikidaiwa Simba ilipanga kumpa Sh 25 milioni na angelipwa mshahara wa Sh 800,000.

Kanuni ya TFF
Kanuni ya 43 ya TFF ya masharti ya mikataba kati ya wachezaji na klabu kifungu cha 3 kinasema; " Klabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu klabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji huyo wa kulipwa.

Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kuingia mkataba na klabu nyingine iwapo mkataba wake na klabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita. Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa."

Tafsiri ya kanuni
Kutokana na kanuni hiyo, Yondani alikuwa huru kufanya mazungumzo au hata kusaini mkataba na klabu yoyote tangu Desemba mwaka jana kwa sababu mkataba wake ulikuwa umebakiza miezi sita kwani umekwisha Mei 31 mwaka huu.

KENYA "SAITOT'S CHOPPER CRASH" - NO ORDINARY ACCIDENT

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
At the addressing of a news conference at Parliament Buildings in Nairobi,  Kenya MPs have expressed their feelings that  there is a scent of  `foul play` surrounding the fatal crash of Police helicopter that killed Kenya Internal Security Minister George Saitoti, his assistant Joshua Orwa Ojodeh and four other government officials,and gave notice of their intention to set up a select committee to conduct parallel investigations.

 MPs expressed doubts that the police chopper crash "was an ordinary accident." They said previous inquiries of similar incidences have been "shoddy".Kenya  National Assembly Speaker Kenneth Marende said a motion has already been filed seeking to create the select committee. On Monday, the government formed a committee headed by Kenya Court of Appeal Judge Kalpana Rawal to investigate the helicopter crash.

 Juja MP William Kabogo, who said he is a trained pilot, doubted that the crash was due to fog or pilot error and called for thorough investigations and compensation for the victims. “As a helicopter pilot, I am not fully convinced about the story we are being given,” said Kabogo. He said there was no way two pilots could have been in confusion for four minutes prior to the crash

 Kilgoris MP Gideon Konchella said the inquest should be held to answer the questions that the public is asking about the helicopter crash.“As far as we are concerned, there are more questions than answers. We’d want to know who serviced the aircraft, if it was serviced; what instruments are inbuilt in it?


“Why was it flying so low? Why did it turn back when we all know that a helicopter can land anywhere? Was someone controlling the aircraft from somewhere else?” Mr Konchella posed

.Mr Konchella said that he flew with Prof Saitoti a few weeks back and he was told that pilots fly to Rironi to get the bearings to Bomet and Ndhiwa, and that there was no point of the helicopter going to Ngong.


 Mathira MP Ephraim Maina who owns a helicopter, said that the bits and pieces surrounding the helicopter crash did not add up.
“As a frequent flyer in a helicopter, I have my doubts. What is this that happened so suddenly that the pilot of the aircraft was not even able to contact the control tower?
“How did the helicopter just come down like a stone?” posed Mr Maina, who is also the chairman of the Central Kenya Parliamentary Group. He said there was no point in having an inquiry that does not reveal the “truth”.
He said the government should get certified aircraft investigators to lead the inquiry.

Narok South MP Nkoidila ole Lankas labelled the accident mystery and called for “thorough, exhaustive and convincing” investigations.
“This crash is not ordinary; it is not normal; there are a lot of grey areas that need to be covered. This should be looked at from all angles,” Mr Lankas said. He took issue with the government call for calm.
“You cannot intimidate people by telling them ‘don’t talk’ yet you’re not giving them answers,” he said.

 Elsewhere, Eldoret North MP William Ruto, who led more than 20 Rift Valley MPs in consoling the bereaved families said any investigations carried out should address all suspicions and answer all questions, “No stone should be left unturned until the truth is known. All questions must be answered,” said Ruto.

  The idea of a parallel investigation was supported by Heritage minister William ole Ntimama who also said  families of the victims should also be involved

.Similar sentiments were echoed by Kisumu Town West MP Olago Aluoch and the Defence assistant minister Joseph Nkaissery who is the MP for Kajiado Central. “The government has a duty to ensure we get to the bottom of this. We want the government to come up with a clear report,” said Nkaissery. Jakoyo Midiwo (Gem) said the investigations should be credible. He said Transport Minister Amos Kimunya should have reconvened the committee that investigated the 2003 Busia plane crash as its members were aviation experts and produced a credible report. The committee was set up to investigate the Busia crash in which then Labour minister Ahmed Khalif died and several other ministers and MPs were injured.

Charles Kilonzo (Yatta) raised questions about the quality of aircraft the government was allocating to fly government officials and said their service and maintenance records should be scrutinised. He expressed concern that some of the choppers and planes still in use might be as old as 30 years. Najib Balala (Mvita) told the House that at least 15 MPs including ministers have died through air crashes since 2003 and said it was time to review the policy on VIP transport.
Preliminary investigators accumulate clues from crash scene

  Technical data of the plane from the manufacturer show that the AS350 B3e police air-wing helicopter was equipped with an instrument used in relaying signals to the control tower.
Aviation experts said that data transmitted to the control tower by the gadget known as a transponder would provide investigators with clues on how the plane went down.
“A transponder gives signals to the people on the ground where the plane is and the height it is cruising at. For example it shows that the plane is 60 miles away cruising at 30,000 feet,” a pilot, who did not wish to be named, said.
He added that a blackbox was normally fitted on commercial planes, but it was an expensive installation for non-commercial aircraft. The Police Air Wing Commandant Rodgers Mbithi told  press on Tuesday that the ill-fated plane was not fitted with a black box.
“This type of a helicopter is small and did not have the black box,” Mr Mbithi said. According to the technical data of the plane from the manufacturer, other instruments and avionics include altitude encoder, emergency locator transmitter, fire detection system, air-intake protection grids and altimeter.



 Mr Mbithi also explained that the police helicopter was bought through open and competitive tender. “The tender was floated last year for companies that met the qualifications,” he said.

The funeral committee chaired by Kenya Vice President Kalonzo Musyoka yesterday proposed that Prof Saitoti be buried on Saturday and Ojode on Sunday. The committee headed by acting head of the civil service Francis Kimemia held its first sitting on Tuesday and  met again Wednesday morning to confirm the dates. Others at the meeting included Cabinet ministers James Orengo, Amos Kimunya, Naomi Shaban, Dalmas Otieno and Wycliffe Oparanya, assistant ministers Gideon Konchellah and Joseph Nkaissery and permanent secretaries Bitange Ndemo, Ludeki Chweya, Mutea Iringo and Andrew Mondoh.

Kenya Prime Minister Raila Odinga has asked the families of the six victims to nominate a representative to the investigations committee headed by Justice Rawal. “The government has constituted a team. The families are free to appoint representatives to sit on the team and take care of their interests,” Raila said. Several ministers and MPs  continued to visit the homes of the six crash victims.

At the CID Training School in Nairobi, the four police officers — pilot Superintendent Nancy Gituanja, her co-pilot Luke Oyugi and Saitoti's bodyguards Inspector Joshua Tongei and Sergeant Thomas Murimi — were awarded Bravery Awards and Wound Stripe Awards by the Manu Chandaria Foundation. Police Commissioner Mathew Iteere and industrialist Manu Chandaria presented the families of the officers with the awards and certificates of merit.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat