StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

June 25, 2012

SAKATA LA MGOMO MADAKTARI: HALI TETE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Sakata la mgomo uliotangazwa na madaktari katika hospitali zote za serikali nchini huenda makali yake yakaongezeka na kuleta athari kwa wagojwa, baada ya Jumuiya ya Madaktari kusema kuwa huduma zote za dharura zitasitishwa kwenye hospitali zote nchini kuanzia leo.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dk. Stephen Ulimboka, alisema jana kwa njia ya simu kuwa, huduma za dharura zitasitishwa katika hospitali hizo kutokana na serikali kutoonyesha nia ya kutatua madai yao kama ilivyotoa ahadi na badala yake kinachofanyika ni propaganda tu.
Dk. Ulimboka alisema wanashangaa kusikia kuwa serikali imeweka zuio mahakamani kushinikiza madaktari wasigome, hatua ambayo alidai ni propaganda tu zinazofanywa na serikali kwani madaktari hawajapewa rasmi taarifa hizo.


“Kauli za serikali na zuio la mahakama tunazichukulia kama ni propaganda tu, kwanza sababu hilo zuio hatujalipata rasmi zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari, kwa hali hiyo kesho (leo) wagonjwa watakuwa na wakati mgumu sana, maana tumekusudia kusitisha huduma zote za dharura katika hospitali zote nchini, ” alisema.

Alisema ufumbuzi wa mgogoro wa madaktari na serikali unashindwa kupatikana haraka kwa sababu viongozi wakuu wa serikali wanaelezwa mambo ya uongo na watu wa chini jambo linalopelekea kutokuwa na habari sahihi za utekelezaji wa madai yao.

Alisema kutokana na serikali kupuuza madai yao italazimika kuwajibika kikatiba katika suala la kuwahudumia wagonjwa ambao wataendelea kupata tabu kwa kukosa huduma za matibabu.

HUDUMA za matibabu kwa wagonjwa jana ziliendelea kuzorota katika baadhi ya hospitali, hali iliyotajwa kuwa inatokana na mgomo uliotangazwa na madaktari.Madaktari walitangaza mgomo wa kutotoa matibabu nchi nzima kuanzia juzi, wakishinikiza Serikali kutekeleza madai yao likiwamo la kuboreshewa mishahara na mazingira ya kazi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),Taasisi ya Mifupa (MOI) na hospitali nyingine za Jiji la Dar es Salaam, umebaini kuzorota kwa utoaji huduma.
Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, uchunguzi ulibaini mbali na ulinzi kuimarishwa, huduma za matibabu kwa wagonjwa zilizorota, na katika baadhi ya wodi wagonjwa walikuwa hawajatembelewa na madaktari tangu Ijumaa.
Mmoja wa watu ambao wanauguza mgonjwa wao katika wodi namba 4 katika Jengo la Mwaisela, Vicky Rehani alisema mgonjwa wao alipelekwa hospitalini Ijumaa na hadi jana, alikuwa hajapata huduma yoyote akiwa wodini.

"Mapokezi kweli alionana na daktari akamuandikia dawa na kulazwa katika wodi hii, lakini cha ajabu hadi sasa hakuna huduma yoyote ambayo ameipata," alisema .
Katika wodi zilizopo katika Jengo la Kibasila baadhi ya wagonjwa walidai kuwa, kuna madaktari ambao wamefika wodini, lakini hawakufanya mzunguko kama ilivyo kawaida, na hawakuwa na wasaidizi wao ambao ni wanafunzi wanaokuwa katika mafunzo kwa vitendo.
Daktari mmoja aliyekutwa katika wodi ya Sewahaji (alikataa kutaja jina lake), alipoulizwa kuhusiana na kuwapo kwa mgomo alikataa kusema lolote kwa madai kuwa si Msemaji wa MNH.
"Siwezi kusema lolote, kwani hata mimi mwenyewe nimefuata matibabu," alisema daktari huyo na kuongeza kuwa kama mwandishi anataka kujua kama kuna mgomo au la, basi aende hospitalini hapo kesho.
Hata hivyo, uchunguzi zaidi hospitalini hapo umebaini kupigwa marufuku kwa mikusanyiko ya aina yoyote na hata bustani inayotumiwa na wagonjwa na jamaa zao ambayo ipo mbele ya Jengo la Mwaisela, ilikuwa chini ya ulinzi.
"Hapa haruhusiwi mtu yeyote kukaa, amri hiyo imetoka tangu jana (juzi)," alisema mlinzi aliyekutwa eneo hilo na kuongeza kwamba hata mikusanyiko ambayo haieleweki imepigwa marufuku ndani ya eneo la hospitali.
Hali hiyo pia iliwakuta baadhi ya waandishi wa habari ambao walifika hospitalini hapo na kujikuta wakizuiwa na walinzi kuingia katika baadhi ya wodi.
Msemaji wa Hospitali hiyo, Aminieli Eligaesha wakati wote simu yake ilipokuwa ilikuwa inaita bila kupokelewa, hali ambayo ilijitokeza pia juzi Jumamosi.
Wakati hali ikiwa hivyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Moi, uchunguzi uliofanywa katika Hospitali za Mwananyamala, Amana na Temeke ulibaini kuwa huduma ziliendelea kwa kusuasua huku baadhi ya wahudumu wakisisitiza hatma ya mgomo huo itafahamika leo.
“Ukitaka kujua sura ya mgomo subiri kesho (leo) itadhihirika kama kweli madaktari wamegoma au la, lakini kwa leo huduma zinaendelea kwa kusuasua, bado tunaangalia Serikali itatoa majibu gani,” alisema mmoja wa madaktari katika Hospitali ya Amana, ambaye hakutaka jina lake kutajwa.
Aliongeza kuwa jana haikuwa siku ya kugoma, bali ni kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao na kwamba, kama itaendelea na msimamo wake huduma zote zikiwamo za dharura zitasitishwa.
Hata hivyo, huduma katika Hospitali ya Amana jana zilikuwa zikiendelea huku baadhi ya wagonjwa wakisema kasi ya upatikanaji matibabu ni tofauti na kipindi ambacho mgomo ulikuwa haujatangazwa.
Katika Hospitali ya Mwananyamala, hali ya matibabu pia iliendelea kwa kusuasua na ulipotafutwa uongozi wa hospitali hiyo kuzungumuzia hali hiyo juhudi hizo hazikuzaa matanda.
Katika Ofisi ya Utawala, mwandishi alikutana na mmoja wa wafanyakazi ambaye alikataa kutaja jina na kueleza kuwa Mganga Mkuu alikuwa amekwenda kutembelea wagonjwa wodini.
“Mimi si msemaji. Hili anaweza kuzungumza Mganga Mkuu, lakini amekwenda kutembelea wagonjwa wodini na ameniambia akimaliza kazi hiyo anakwenda kufanya shughuli ya upasuaji, hatakuwa na muda wa kuzungumza nanyi,” alisema ofisa huyo.
Wakati hali ikiwa hivyo Mwananyamala, katika Hospitali ya Temeke pia huduma ziliendelea kutolewa huku baadhi ya watu waliokwenda kuhudumia wagonjwa wao wakibainisha kuwa kasi imepungua.
Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Edwin Chitage alisisitiza, “Sisi tunaendelea na mgomo kama kawaida, tutafanya hivyo hadi Serikali itakapotekeleza madai yetu, na hadi sasa hatujapata taarifa zozote kutoka serikalini,” alisema Chitage.

KCMC vuguvugu laendelea
 Katika Hospitali ya Rufaa KCMC Moshi, madaktari ambao hawako zamu wamekubaliana kufanya kikao cha dharura kuhakikisha hakuna daktari atakayeingia kazini leo.

Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya madaktari ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, walisema wamepanga kufanya kikao cha pamoja ambacho kitaweka mikakati ya jinsi ya kufanya mgomo mkali leo, tofauti na ilivyokuwa juzi na jana.

“Mgomo uko palepale kama unavyoona walioko kazini ni wale wenye zamu, tumewataka wasaini, lakini kesho hakuna atakayeingia kazini na mgomo utakua mkali, tumekuwa wapole sana, lakini Serikali imetupuuzia,” alisema mmoja wa madaktari.

Chama cha Tiba Asilia
Kwa upande wa Chama cha Watabibu wa Dawa za Asili (ATME), kimewataka madaktari kuacha kugoma na badala yake waendeleze mazungumzo na Serikali ili waweze kufikia muafaka.

Chama hicho kupitia Mwenyekiti wake, Abudulhaman Simba, kimesema mgomo wa madaktari unahatarisha uchumi wa taifa na haki za wagonjwa, hasa wale wenye kipato cha chini.

Mkoa wa Mwanza
Mkoani Mwanza madaktari walio kwenye mafunzo na wale walioajiriwa waliendelea na mgomo wao jana.

Mmoja wa madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa Bugando ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema mgomo huo kwa sasa haujaonyesha athari kubwa kutokana na kuwa siku za mapumziko.

"Leo (jana) na jana (juzi), hapajatokea athari za mgomo, tunadhani athari itakuwa kubwa katika siku za kesho (leo) na kuendelea kwani wakigoma hawa wa mafunzo na hao wengine, kazi inakuwa kubwa kwetu," alisema.

Katika hatua nyingine, mgomo huo haukugusa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwani huduma ziliendelea kama kawaida.

Gazeti hili jana lilishuhudia wagonjwa wakipewa huduma za matibabu pamoja na mgomo uliotangazwa kudai maslahi yao.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk Omary Chande alisema pamoja na kutangazwa mgomo wa madaktari, Mount Meru haijaathirika na mgomo huo.

Wagonjwa waondolewa Mbeya
Katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, mgomo uliendelea na kusababisha baadhi ya wagonjwa kuanza kuondolewa hospitani hapo pia na ile ya wazazi, Meta, kwa ajili ya kwenda kutafuta matibabu kwenye hospitali nyingine za watu binafsi.
Mwananchi jana lilishuhudia baadhi ya wagonjwa wakipandishwa kwenye magari na kuondoka kwenda kutafuta matibabu hospitali za watu binafsi.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk Eliuter Samky alipoulizwa alikiri kuwepo kwa mgomo wa madaktari walio kwenye mafunzo ya vitendo wanaofikia 70.
Hata hivyo, Dk Samky alisema anao uhakika kuwa madaktari 10 bingwa waliojariwa na Serikali wataendelea kufanya kazi, na hivyo huduma kwa wagonjwa hasa wale walio katika hali ngumu na wale wa dharura zitaendelea kupatikana.
Ombi la wagonjwa
Wagonjwa jijini Tanga,wameiomba Serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa madaktari ili kuondoa misunguano iliyojitokeza.

Ombi hilo walilitoa jana walipokuwa wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi katika wodi za majeruhi na watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo.

"Tunamuomba Rais atekeleze ahadi yake aliyotoa kwa madaktari, wanapogoma sisi walalahoi ndo tunaokufa na wengine kupata madhara zaidi, lakini wao wanapougua wanakwenda hospitali za nje ya nchi," alisema Adamu Abdurahman aliyelazwa katika wodi ya majeruhi ya
Galanosi.

Madaktari waliokuwa zamu katika wodi za Hospitali hiyo walisema hawaamini kama kweli Serikali haina fedha za kuwalipa, kwani kunapotokea masuala mengine imekuwa ikitoa bila ya matatizo.


HUDUMA MUHIMBILI ZASUASUA

Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jana utoaji wa huduma kwa wagonjwa zilikuwa zikisuasua ambapo wagonjwa walieleza hali hiyo ilianza kujitokeza tangu juzi.

Katika wodi ya watoto, wauguzi waliokuwa wanaonekana wakifanya kazi ni wale walioitwa kwa dharura na wengi wa madaktari hawakuonekana katika sehemu zao za kazi.
Mmoja wa daktari katika wodi hiyo, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema, wameamua kusitisha huduma mpaka serikali itakaposikiliza hoja zao za msingi.
Alisema watoto wengi wanakufa kwa ukosefu wa hewa ya oksijeni wanapofanyiwa upasuaji kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuvutia hewa.
Alisema kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kutatua matatizo yanayowakabili madaktari imekuwa ikidharau vikao hivyo, na kila siku wanapokutana kunakuwa na watu wengine tofauti na wale waliokutana nao awali.

“Kila kikao tunachokaa na wawakilishi kutoka serikalini wanakuwa wapya, kikao hiki wanakuja hawa, kikao kinachofuata wanakuja wengine wapya, jambo linalopelekea kutopiga hatua katika mwafaka,” alisema daktari huyo.
Daktari huyo alisema wanamshangaa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi kwa kauli yake ya kusema anataka kuzungumza na madaktari upya wakati anafahamu kuwa mazungumzo na serikali yameshafanyika mara kadhaa bila ya kuafikiana madai yao.


HOSPITALI YA TEMEKE
Msimamizi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Rolesta Kinunda, alisema hakuna mgomo kwa madaktari wanaendelea na kazi kama kawaida na wanaendelea kupokea wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Huduma katika hospitali hiyo zilionekana kuendelea kama kawaida, ambapo madaktari walionekana wakipita wodini na kutoa huduma kama kawaida.
Rashid Ndwangila, mkazi wa Mbagala, ambaye amelazwa kwenye wodi namba saba ya wanaume hospitalini hapo baada ya kufanyiwa operesheni ya henia alisema kwa jana madaktari walipita kama kawaida na kuwahudumia wagonjwa wote kwa kuwapatia dawa pamoja na kuwafunga vidonda.


AMANA NA MWANANYAMALA
Huduma katika hospitali hizo zilionekana kuendelea kama kawaida ambapo wagonjwa walikuwa wakihudumiwa na madaktari.


MBEYA: JAMAA WAONDOA WAGONJWA 
Baadhi ya jamaa wa wagonjwa wameanza kuwaondoa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa ajili ya kwenda kutafuta matibabu kwenye hospitali za watu binafsi.


NIPASHE jana liliwashuhudia baadhi ya wagonjwa wakipandishwa kwenye magari na kuondoka kwenda kusikojulikana.


Averine Ngeya, mzazi wa mtoto Miliam Alex ambaye ameungua vibaya kwa maji ya moto, alisema tangu juzi baada ya madaktari kuanza mgomo, wagonjwa hawapati huduma nzuri za matibabu zaidi ya kupewa na wauguzi vidonge vya kutuliza maumivu.


“Tangu jana (juzi) hakuna matibabu ya maana ambayo mwanangu ameyapata, wauguzi ndio wanatupatia panado za kutuliza maumivu na kutuambia kuwa tusubiri daktari anaweza kuja wakati wowote, lakini madaktari hawatokei,” alisema Ngeya.


Nipashe limetembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Wazazi iliyopo eneo la Meta mjini hapa na kushuhudia eneo la hospitali likiwa halina watu kutokana na matangazo yaliyobandikwa kwenye mbao za matangazo na kuta za hospitali hiyo yakionyesha kuwa hakuna huduma.


Ofisi za hospitali hiyo na ile ya rufaa zilikuwa zimefungwa na wauguzi waliokuwa vibarazani walikataa kuzungumza lolote kuhusiana na hali hiyo kwa madai kuwa wao sio wasemaji.


Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk. Eliuter Samky, alithibitisha kuwepo kwa mgomo wa madaktari walio kwenye mafunzo ya vitendo wanaofikia 70.


Hata hivyo, alisema anao uhakika kuwa madaktari 10 bingwa wataendelea kufanya kazi na hivyo huduma kwa wagonjwa hasa wale walio katika hali ngumu na wale wa dharura zitaendelea.


KCMC WAENDELEA KUGOMA


Mgomo huo umeiathiri Hspitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, ambapo inasemekana kila idara ina
daktari mmoja wa zamu huku wengi wakiwa kwenye mgomo.


Habari ambazo zimethibitishwa na baadhi ya madaktari waliopo kwenye mgomo zinasema sio rahisi kubaini athari kwa kuwa jana ilikuwa siku ya mapumziko.


“Kuanzia leo (kesho) ndio athari za mgomo wetu zitaonekana vizuri, kwani tutaachia maeneo yote na kubakiza eneo la wagonjwa mahututi na majeruhi wa ajali mbalimbali,” alisema daktari mmoja na kuongeza: “Lengo si kuwaumiza wananchi bali kuishinikiza serikali kutekeleza madai yetu.”


Mwanahamisi Ally aliyelazwa wodi ya majeruhi na Haji Rashidi anayemuhudumia baba yake katika wodi namba mbili, walisema huduma si za kuridhisha sana kwani kuna mabadiliko ya wazi tangu madaktari walivyotangaza mgomo na wanaoumia zaidi ni wagonjwa, madaktari hawaonekani wakitoa huduma na hata wakihitajiwa hawaonekani.

“Tunaiomba serikali kumaliza tatizo hili kwa haraka, sidhani kama mahakama inaweza kuwa ndiyo suluhisho la kushinikiza madaktari warudi kazini, wakirudi kwa mtindo huo hali haitakuwa nzuri,” alisema Rashid.

DODOMA 34 WAGOMA

Madaktari 34 walioko katika mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma, juzi hawakufika kazini licha ya kutakiwa kuwepo.

Hata hivyo, huduma  katika hospitali hiyo na Kituo cha Afya cha Makole zilikuwa zikiendelea kama kawaida.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.  Ezeckiel Mpuya, alisema wameendelea na huduma za matibabu kama kawaida katika hospitali yao.

MGOMO BUGANDO WATHIBITISHWA

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza umetihibitisha baadhi ya madaktari wake kuanza mgomo rasmi.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk. Japhet Gilyoma, ameliambia NIPASHE jana kuwa, licha ya mgomo huo kuanza, lakini hali ya huduma za matibabu bado si mbaya sana kwa sababu kuna madaktari bingwa ambao waliendelea kuhudumia wagonjwa juzi na jana.

“Ni kweli kwamba madaktari wetu pia wameingia katika mgomo, lakini kama unavyojua leo(jana ) ni weekend (mwisho wa juma) madaktari wanaokuwa zamu ni wachache, ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba hali ya matibabu si mbaya kwa sababu specialists (madaktari bingwa) wanaendelea na matibabu, ” alisema.

TANGA SHWARI

Katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga  ya Bombo, jana madaktari waliokekana wakiwa wanatoa huduma za katibabu kwa wagonjwa kama kawaida.

Miss Reds Arusha 2012: Warid Frank aibuka kidedea

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Reds miss arusha 2012 Warid Frank
 warembo walioingia top 5
 mshindi wa tatu anitha sebastian akipita na vazi la ubunifu
mshindi wa pili sarah benjamin akipita na vazi la ubunifu
Reds miss arusha 2012 akipita na vazi la ubunifu
wasanii mbalimbali wakitumbuiza

Mashindano ya  Reds miss Arusha 2012 yaliurindima ktk ukumbi wa Mount Meru Hotel iliyopo eneo la Sekei Arusha ambapo Miss Warid Frank alibuka mshindi akifuatiwa na Sarah Benjamin aliyekuwa mshindi wa pili, na Anitha Sebastian aliyeshika nafasi ya tatu.
Aidha pia mashindano hayo yalisindikizwa na wanamuziki mbalimbali akiwamo Diamond, Sam wa ukweli na wengineo...

Breaking News:Benz ML class lateketea kwa moto!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Muda mfupi uliopita moto umeteketeza gari aina ya Mercedes Benz ML Class ambalo namba zake hazikupatikana mara moja baada ya moto kuwa mkubwa, Gari hilo lilipoteza mwelekeo na kuingia mtaroni na kushika moto. Ajali hiyo imetokea  katika barabara ya Kilwa eneo la Tanesco, Mivinjeni. Mmoja wa mashuhuda ambaye alikuwa na gari lingine nyuma ya gari hilo kabla ya ajali, amesema dereva wa gari hilo alikuwa akiongea na simu kabla ya ajali hiyo!

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa refa wa mchezo wa soka kati ya wabunge mashabiki wa Simba dhidi ya Yanga.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa refa wa mchezo wa soka kati ya wabunge mashabiki wa Simba dhidi ya Yanga.
Mechi ya wabunge hao mashabiki wa Simba na Yanga, inatarajiwa kufanyika Julai 7, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya matukio yatakayopamba Tamasha la Usiku wa Tumaini.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, wanaoandaa tamasha hilo, Abdallah Mrisho, alisema kuwa wameshamuandikia barua JK ya kumuomba awe mgeni rasmi, vilevile awe refa wa mechi hiyo ya wabunge na kwamba matarajio ni mazuri.
“Tuna matarajio ambayo ni chanya kuhusu Mheshimiwa Rais kuingia uwanjani na kuchezesha mechi ya wabunge na kwa kweli hili litakuwa tukio la kihistoria kuwahi kutokea,” alisema Mrisho na kuongeza:
“Tunaamini kwamba kitendo Mheshimiwa Rais kuchezesha mechi hiyo ya wabunge, siyo tu kwamba kitawafurahisha wananchi watakaohudhuria tamasha hilo la Usiku wa Tumaini, bali pia kitakuwa faraja kubwa kwa kila mhudhuriaji na Watanzania kwa jumla.”
Katika tamasha hilo, mbali na mechi ya wabunge, kutakuwa na mchezo wa soka kati ya wasanii wa filamu Tanzania (Bongo Movie) dhidi ya wenzao wa muziki (Bongo Fleva). Vilevile wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo, watachuana na wenzao wa Shule ya Sekondari Jitegemee.
Upande wa masumbwi, bondia Francis Cheka atamaliza ubishi na Japhet Kaseba, ikikumbukwa kwamba mara ya mwisho walipopigana, pambano lao halikufika mwisho.
Kuhusu burudani, wanamuziki wakali jukwaani, Joseph Mayanja ‘Chameleone’ na Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ watapambana kuoneshani ni nani anatisha kwa kumiliki ‘steji’ ukanda wa Afrika Mashariki.
Wakali wa Hip Hop, Ibrahim Mussa ‘Roma’, Rashid Makwilo ‘Chidi Benz’, Kundi la Pah One na wengine wengi watakuwepo.
Source; Global Publishers Info

WEMA & OMOTOLA WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends


Mchezaji wa Filamu kutoka nchini Naigeria Omotola Jalade katikati akiwa katika picha ya pamoja na mwigizaji Wema Sepetu kushoto na Khadija Mwanamboka pamoja na watoto yatima wa kituo cha Tanzania Mitindo House cha jijini Dar es salaam Omotola amekuja nchini maalum kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu Super Star ambayo imezinduliwa jana kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam 

Mohammed Mursi Aibuka Kidedea Uchaguzi Wa Misri

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Mursi ameshinda kura kwa asili mia 51.7% akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.


Mkuu wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko 466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika.


Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi wengi wa Bw.Mursi walikua wamekuanyika.


Wafuasi hao wamekaa kwenye medani hio kwa siku kadhaa wakionyesha msimamo wao wa kuchukia sheria kadhaa zilizotangazwa na Baraza la juu la utawala wa majeshi ambayo wanadai zimeundwa ili kupunguza mamlaka ya Rais na kuelekeza uwezo mkubwa kwa majeshi.


Wafuasi wa Bw.Shafiq nao waliweka kambi yao katika eneo la kaskazini mwa mji ambako kuna makao makuu ya Tume ya uchaguzi huko Nasser City.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi Jaji Sultan alianza kwa kunena kua tangazo la matokeo ya uchaguzi yalikua yamezongwa na shinikizo pamoja na hali ya wasiwasi.


Tume ya uchaguzi ilizingatia sheria ilipochunguza visanduku vya kupigia kura, na Jaji.Sultan alisema hakuna kilicho juu ya sheria.

Jaji huyo akaongezea kukanusha madai mawili nyeti kuhusu njama za kuibia uchaguzi, kwamba baadhi ya karatasi za kupigia kura ziliwekwa ndani ya visanduku tayari zikiwa na majina ya mgombea wanayemtaka ashinde.


Hatimaye Jaji Sultan akamtangaza mshindi kua ni Bw.Mursi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Muslim Brotherhood cha Freedom and Justice, Bw.Mursi.


Baada ya dakika kadhaa akitangaza marekebisho kuhusu matokeo madomadogo ya kura ndipo akamtangaza Bw.Mursi kua mshindi kwa kuzoa kura 13,230,131, na Bw.Shafiq akiweza kuzoa 12,347,380, sawa na asili mia 48.27%.
Chanzo: bbc swahili.  http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

MICHUANO YA OLIMPIKI LONDON 2012

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Jiji la London litakuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka 2012 ya Olimpiki. Je London imejiandaa vipi na michuano hiyo? fuatilia maandalizi na matayarisho ya viwanja na wachezaji

Aidha pia Kamati ya maandalizi ya olympiki London 2012 imesema mfumo wake wa uuzaji tiketi za michuano ya Olimpiki wa mara ya pili utaanza tena hivi karibuni

Waziri mkuu mtarajiwa Pakistan kukamatwa

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Jaji mmoja nchini pakistan ametoa kibali cha kukamatwa kwa Makhdoom Shahabuddin, ambaye ametajwa na serikali ya nchi hiyo kama mgombea anayeungwa mkono na wengi kuwa waziri mkuu mpya.
Kibali hicho kimehusiana na uagizaji wa dawa za hospitalini wakati Shahabudin akiwa waziri wa afya.
Bwana Shahabuddin ni mmoja wa maafisa wakuu wa chama cha Pakistan People's Party ambacho kinaongoza serikali ya sasa ya mseto.
Bunge la nchi hiyo linatarajiwa kumuidhinisha rasmi hapo kesho kuwa waziri mkuu.
Uamuzi huo wa mahakama ni tukio la hivi karibuni, linalothibitisha uhasama kati ya idara ya mahama na serikali ya nchi hiyo.

Mji wa Mombasa washambuliwa kwa mabomu.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mtu mmoja ameuwaa na wengine kujeruhiwa na mabomu mjini Mombasa siku moja baada ya onyo kutolewa na  ofisi za ubalozi wa Marekani. 
Polisi mjini Mombasa imesema " mashambulizi hayo yalitokea saa nne usiku kwa muda wa masaa ya Kenya wakati wakazi wa mji huo wanaangalia mshindano ya kombe la Ulaya kwenye bar moja iliyopo Mombasa mjini."
Onyo la mashambulizi katika mji wa Mombasa, lilitiliwa maanani na kuzifanya serikali za nchi za Magharibi kuwaonya wananchi wao kuwa waangalifu watakapo kuwa katika matembezi ya kitalii katika mji wa Mombasa.

MAELFU WAMZIKA WILLY EDWARD OBUNDE

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
MWILI wa aliyekuwa mhariri mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Obunde, umezikwa leo nyumbani kwao katika kijiji Morotonga, nje kidogo ya mji wa Mugumu mkoani Mara.
Mazishi ya mhariri huyo, yalihudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, waandishi wa habari, viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti kapteni mstaafu James Ryamungu, viongozi wa vyama vya siasa, madhebu ya dini, pamoja na wananchi mbalimbali.
Aidha, mazishi ya mhariri huyo, pia yalihudhuriwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mngeja pamoja Mkuu mpya wa Wilaya ya Magu, ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, Jacqline Liana. 
Ibada ya mazishi hayo, iliongozwa na Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilkiah Omindo, ambaye aliwataka wananchi kujiandaa kwa kufanya matendo mema na kumtumikia Mwenyezi Mungu.
Akitoa salamu kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, Mwenyekiti wa CCM, mkoani Shinyanga, Khamisi Mngeja, amesema kuwa waandishi wa habari wamepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mwenzao ambaye alikuwa ni mchapakazi, mwadilifu na anayefuata maadili na weledi wa uandishi wa habari.
Willy Edwar (38), alifariki dunia ghafula akiwa mkoani Morogoro, usiku wa kuamkia juni 17, mwaka huu, wakati akiwa kwenye semina ya uandishi wa habari za Sensa ya watu na makazi.
Marehemu Willy Edward, alikuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo na ameacha watoto watatu na mjane mmoja, Mungu alitoa na Mungu ametwaa, jina la Mungu iliimidiwe, na hivyo tunaomba aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.




MAKALA: Kila mwaka? Kama ndivyo, basi!

Tweeted this Like this, be the first of your Friends SASA bia wanywe wao. Soda wanywe wao. Sigara wavute wao. Sisi basi. Ebo! Hivi hapa ndipo mahali pekee ambako serikali inaweza kupata fedha za bajeti?
Twende kwenye bia. Kama serikali inajali, kwanini isiteremshe bei ya bia. Ili watu wengi waweze kunywa au watu walewale waweze kunywa bia nyingi.
Ili kampuni ziweze kutengeneza bia nyingi. Ili kampuni zipate mapato makubwa. Ili kampuni ziweze kulipa kodi kubwa. Ili serikali iweze kunufaika kwa kodi kubwa. Kwanini?
Twende kwenye soda. Kama serikali inajali, kwanini isiteremshe bei ya soda. Ili watu wengi waweze kunywa au watu walewale waweze kunywa soda nyingi.
Ili kampuni ziweze kutengeneza soda nyingi. Ili kampuni zipate mapato makubwa. Ili kampuni ziweze kulipa kodi kubwa. Ili serikali iweze kunufaika kwa kodi kubwa. Kwanini?
Twende kwenye sigara. Kama serikali inajali, kwanini isiteremshe bei ya sigara. Ili watu wengi waweze kuvuta au watu walewale waweze kuvuta sigara nyingi.
Ili kampuni ziweze kutengeneza sigara nyingi. Ili kampuni zipate mapato makubwa. Ili kampuni ziweze kulipa kodi kubwa. Ili serikali iweze kunufaika kwa kodi kubwa. Kwanini?
Sasa wanywaji hawana hamu tena! Ama serikali inywewe bia; inywe soda na ivute sigara. Au wavitumie wanaovitengeneza.
Huo hapo juu waweza kuonekana kama muweweseko wa wanywaji soda, bia na wavuta sigara; bila kujua uchumi wa uzalishaji na masoko. Lakini kwa viwango vyovyote vile, kuna mantiki.
Ukitokea mgomo wa “kunywa” na “kuvuta,” mwezi wa sita wa mwaka wowote ule, nchi ikiwa chini ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), bajeti haitasomwa kamwe. Haitakamilika.
Kila mwaka ni bia, soda na sigara; hadi wenye viwanda wakaonya kwamba mwaka huu wakipandishiwa kodi zaidi ya asilimia 10, hawataielewa serikali.
Kujaribu kuonyesha “ubunifu,” serikali imekuja na pendekezo la wanaotaka usajili wa magari kwa utambulisho wa taarifa za mtu binafsi – majina, labda na picha na chochote kile – kulipa Sh. 5 milioni kwa miaka mitatu.
Ni yaleyale ya bia, soda na sigara. Serikali inasema itakusanya Sh. 50 milioni katika miaka mitato; kwa kutoza Sh. 5 milioni kwa atakayetaka urembo.
Hii ina maana serikali imelenga watu 10 tu. Wakilipa milioni 50 kila mmoja, serikali itakuwa imeridhika. Masikini!
Kama serikali inahitaji fedha kwa njia hii, kwanini isitoze Sh. 200,000 kwa mwaka kwa gari kwa maelfu ya magari ya vijana wanaotaka mbwembwe? Itapata zaidi.
Ukiangalia orodha ya magari binafsi yaliyosajiliwa hadi sasa katika mfumo mpya, utaona yametoka AAA hadi CAG. Haya ni maelfu ya magari. Serikali haitaki wanaoyamiliki washiriki.
Kinachoonekana hapa ni kwamba, watunga bajeti wanataka watu wachache (10), na huenda mafisadi wachafu zaidi, wapate nafasi ya kujitambulisha kwa mbwembwe.
Kwamba wezi wakubwa, wenye mabilioni ya shilingi ya kusambaza; mabilioni waliyopora umma wa nchi hii; wapate nafasi ya kuwakoga wananchi na kuonyesha kwamba wao ni tofauti.
Kwamba mafisadi walioshindikana, sasa wapate nafasi ya kurudi upya katika umma, kwa kuutisha, kuushangaza, kuukoga na kuudhalilisha kwa fedha walizowaibia.
Lakini, hata kama kiwango kisingekuwa Sh. 5 milioni, au laki mbili; wazo lenyewe la mikogo, katikati ya umasikini unaoandama wananchi, hakika ni la kibwege sana.
Aliyetoa wazo hilo barazani na “wataalam” walioliunga mkono ili kupata Sh. 50 milioni, wamedhihirisha uchovu mchafu.
Hiki ni kiasi ambacho serikali inaweza kupata katika siku nne tu kutokana na faini kwa makosa ya barabarani katika jiji la Dar es Salaam peke yake!
Serikali yaweza kupata kiasi hiki katika wiki moja au siku saba, kwa kusimamia kwa makini, ukusanyaji kodi kwenye masoko.
Fedha zinazohitajika ili kukidhi mbwembwe za kifisadi, zinaweza kupatikana – tena mara kumi au ishirini au zaidi – kwa siku moja tu, kwa kufuta wilaya moja iliyoundwa kisiasa na isiyo na manufaa kiuchumi kwa wananchi.
Watunga bajeti hawaoni wezi wanaokwapua madini kweupe. Hawaoni mafisadi wenye kodi za wananchi kwenye akaunti zao Ulaya. Hawaoni mabomba yanayovujisha mabilioni ya shilingi kwa njia ya mishahara hewa.
Hawaoni! Hawaoni safari za ndani na nje za watawala zinazokausha hazina na madarasa ya Ngurdoto yanayokamua walipakodi. Hawaoni dege la serikali lilalo mafuta kama ibilisi. Hawaoni!
Si busara kupendekeza serikali isitoze kodi kwenye bia, soda na sigara. Bali hoja ni hii:
Kuna muda mwingi na mrefu wa kuandaa bajeti. Kuna vyanzo lukuki. Kitendo cha serikali kuonekana inakwanyiakwanyia – shika hili shika lile – dakika za mwisho na katika bidhaa zilezile, ni ushahidi watawala wanaishi kama wapitanjia.
Na mpitanjia hajengi.

UDHAIFU WA JK; TAFSIRI YANGU

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 
Ndugu zangu,
Watanzania wengi hatuna mazoea ya kusoma, hata makala za magazetini ukiachilia mbali vitabu vya taarifa na hadithi. Ndio, tu wavivu wa kusoma.
Kigong’onda ni aina ya ndege.  Ndege huyu  ana mdomo mrefu na anapenda sana kugongagonga mti kwa mdomo wake. Ndivyo anavyojipatia ridhiki yake. 
Lakini, kwa hulka yake ya kugong’onda kila kilicho mbele yake, basi, hata ukimwekea mti wa chuma porini, kigong’onda atahangaika nao mpaka damu zimtoke mdomoni. Ni hulka yake.  Kiongozi hapaswi kuwa kama kigong’onda.
Kuna hoja mezani juu ya udhaifu wa JK, imetokea Bungeni.  Yumkini, kama mwanadamu, JK ana mapungufu na udhaifu wake, nani asiye na mapungufu na udhaifu? Lakini, tukimzungumzia JK kama taasisi ya ’ Urais’, namwona Rais anayejipambanua na waliomtangulia. Ni  kwa kujitahidi kufanya yale yalo nafuu na yenye manufaa kwa nchi yetu  kwenye mfumo dhaifu uliopo.  
Wanadamu tunapaswa kuhukumu dhamira ya mtu na si matokeo. Bado namwona JK kama kiongozi mwenye dhamira njema kwa nchi yetu. Nauona ujasiri ndani ya JK. Ni ujasiri wa kufanya yale ambayo, hata ndani ya chama chake hayakuwezekana kufanywa na Mwenyekiti wa chama huko nyuma. Na bila shaka, kuna wahafidhina ndani ya chama chake wanaomwona JK kuwa ni dhaifu kwa mantiki hiyo. Kuna wanaoamini, ndani ya CCM, kuwa Rais wa chama tawala anayekaa na kuongea na wapinzani Ikulu ni Rais dhaifu!
Na hata haya tunayoyashuhudia sasa, yumkini ni matokeo ya dhamira njema ya JK. Naamini, kwa tunavyoenenda sasa, Tanzania atakayoiacha  JK haiwezi tena kurudi kuwa kama ilivyokuwa kwa Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. JK amepanua uhuru wa Watanzania kuchangia fikra zao bila hofu. Siku zote, hofu haijengi nchi.
Maana, tumefika hapa kutokana na mfumo dhaifu unaozaa Serikali dhaifu, unaozaa Bunge dhaifu na unaopelekea pia kuzaa vyama dhaifu vya siasa ikiwamo chama tawala. Na chimbuko lake ni Katiba ya Nchi iliyo DHAIFU. Ndio, tatizo la nchi yetu ni tatizo la kimfumo.
Ni tatizo lililoasisiwa tangu Awamu ya kwanza ya Urais.  Angalia, Katiba yetu inampa nguvu nyingi sana Rais. Tuna bahati tu hajatokea Rais anayeamua kuzitumia ipasavyo nguvu hizo.
Nimeona katuni ya ndugu yangu Masoud Kipanya kwenye gazeti la Mwananchi la jana, Juni 23, 2012.  Kipanya alionyesha foleni ndefu ya wapiga kura Watanzania walio tayari kumpigia kura Rais Dikteta.   
Niliogopeshwa na michango ya  maoni ya Watanzania juu ya katuni ile. Wengi walionekana kuikubali hali hiyo. Kuwa kwao kwa hali ilivyo sasa ni heri kutawaliwa na dikteta kuliko Rais dhaifu!
Inasikitisha na inaogopesha kuona kuwa tumefika hapa. Naamini mimi na wengine wengi tuliokulia enzi za chama kimoja  na Rais mmoja ambaye ni kila kitu, tusingependa kurudi huko tulikotoka. Nikayasoma jukwaa moja maoni ya Mtanzania Ludovic Mwijage aliyejaribu kuonyesha ubaya wa udikteta. Hapo chini nimeweka kitabu cha Mwijage kilicho kwenye maktaba yangu. Kwa mimi niliyesoma kitabu chake, ningeshangaa kama Mwijage angeunga mkono hoja ya kumwona JK dhaifu na kutamani Rais Dikteta.
Ukweli, sisi wa ’ Kizazi Cha Azimio’ tuliwaona wazazi wetu wakiishi katika hali ya hofu na mashaka. Waliishia kunong’ona tu pale walipotaka kuishutumu Serikali na Rais aliye madarakani.
Mjumbe wa nyumba kumi alikuwa ni mtu aliyeogopewa sana.  Huyu  alikuwa ni wakala wa Chama tawala na Serikali. Moja ya majukumu yake ilikuwa ni kuwatambua, katika nyumba zake kumi, wale wote waliokuwa na mitazamo tofauti na ya Serikali na Mkuu wa Nchi. Ni wale walioitwa ’ Wapinga Maendeleo!’. Kuna waliosekwa rumande, kuna waliofungwa magerezani.
Enzi zile viongozi watu wazima walisimama majukwaani na kusema; ” We have a One Party Democracy!” Katika dunia hii hakuna ‘ One Party Democracy’ bali ‘ One Party Dictatorship’. Hata kwenye nyumba mwanamme ukishaoa huwezi tena kutamka juu ya ‘ One Man Family!’- Na watoto wakiingia kwenye familia , nao pia wanatakiwa wawe na sauti.
Afrika Rais anategemea sana wasaidizi wake katika kuifanya kazi yake. Hivyo, mfumo dhaifu huzaa wasaidizi dhaifu pia. Mfano, pale Bungeni hakukuwa na haja yoyote ya mbunge kutolewa nje kwa kutamka ‘ JK ni Dhaifu’.   
Badala yake, ilikuwa fursa kwa wasaidizi wa JK kujenga hoja za kubomoa hoja za mbunge huyo.
Kumtoa Mbunge nje kumemsaidia zaidi kuwasilisha ujumbe wake na hata ukaaminiwa na wengi. Maana, swali la hata wasiofutilia vipindi vya Bunge ni ‘ Kwani huyo Mnyika amesema nini?” Ni yale yale ya Zitto Kabwe kutolewa Bungeni kwa hoja ya Buzwagi. Nakumbuka kumsikia Mzee Malecela akisimama Bungeni na kutamka, kuwa dawa ya kidole chenye kansa ni kukikata!
Malecela na wengine katika CCM walisaidia, kwa kasi ya ajabu, kumtangaza na kumpa umaarufu Zitto Kabwe. Maana, wengi mitaani walitaka kukiona kidole hicho chenye kansa kinachokisumbua chama tawala na kikongwe hapa nchini, CCM.  
Na mpaka hii leo, CCM wanarudia makosa yale yale ya jana. Na kwanini wanarudia? Ni kwa baadhi ya watendaji, kuingiwa hofu na wimbi hili la mabadiliko, hivyo kutojiamini na hata kufanya yale wanayodhani yatamfurahisha aliyewateua, kumbe, wanamharibia, na wanazidi kukipaka matope chapa chao.
Naam, tunaweza kuondokana na mfumo dhaifu kupitia Katiba mpya ijayo. Inawezekana.

Makala hii imeandaliwa na Maggid Mjengwa

KOMBANI: MISHAHARA HAITACHELEWA TENA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imesema hakutakuwapo tena ucheleweshaji mishahara kwa watumishi wapya kutokana na kufungwa kwa mfumo wa mawasiliano ya kompyuta kila taasisi ya umma.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Waziri wa ofisi hiyo, Celina Kombani, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya Utumishi wa Umma yanayoadhimishwa leo.

 Kombani alisema mfumo huo  utawezesha taarifa za watumishi wapya kufika na kufanyiwa kazi haraka na  ofisi ya utumishi, hivyo  kuziwasilisha taarifa zao hazina kwa ajili ya malipo yao.
Alisema kwa sasa kila taasisi ya Serikali nchini imefungiwa mfumo huo wa kompyuta, hivyo wanatakiwa kuingiza taarifa za wafanyakazi wao pale walipo kwa kutumia mtandao.

 “Sasa hivi ukiona mishahara inachelewa basi ujue taarifa za mtumishi aliyeajiriwa zimechelewa kufika utumishi, kwa kuwa zinatakiwa kufika kabla ya tarehe 15 kwa ajili ya kupeleka taarifa hazina ili waandae malipo mwisho wa mwezi,” alisema Kombani.

Mbali na mishahara kutocheleweshwa, huduma hiyo ya mtandao pia itasaidia kupunguza malimbikizo ya madeni kwa watumishi wa umma kwa kuwa taarifa za kila siku za mtumishi zitakuwa zikifika ofisi ya utumishi kwa wakati.

Taarifa hizo ni pamoja na kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi, taarifa za vifo, kuachishwa kazi, likizo na taarifa za wafanyakazi wanaostaafu.

“Mfumo  huu toka umeanzishwa una miezi saba na umeonyesha mafanikio kwa kuwa kwa kiasi kikubwa, suala la malalamiko ya malimbikizo mbalimbali ya watumishi yamepungua ukilinganisha na awali. Tunategemea kuyamaliza kabisa hapo baadaye,” alisema.

Alisema Serikali imeunda Bodi ya Mishahara na Maslahi kwa Watumishi wa Umma, ambayo itakuwa na jukumu la kufanya utafiti juu ya hali ya mishahara ya watumishi wa umma.

Waziri Kombani alisema bodi hiyo itachunguza mishahara ya watumishi wa umma wote na kulinganisha na hali ya uchumi na gharama za maisha, itaanza kazi mwaka huu wa fedha.

Kuhusu maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma, Kombani alisema kaulimbiu ya mwaka huu  ni ‘Kujenga uwezo wa utekelezaji wa mkataba wa misingi na kanuni za utumishi wa umma na utawala, ili kuwa nchi inayojimudu kwa maendeleo Afrika’.

Alisema kama ilivyo kawaida kila mwaka kuadhimisha siku ya Utumishi wa Umma kwa kufanya maonyesho, mwaka huu hayakuwepo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kubana matumizi ya fedha za umma.

MADAKTARI WAANZA MGOMO RASMI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
MADAKTARI nchini wameanza mgomo katika baadhi ya hospitali nchini baada ya Serikali kushindwa kutekeleza madai yao waliyowasilisha katika Kamati ya Majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.  Mgomo huo umetangazwa na Jumuiya ya Madaktari nchini huku ikifafanua kwamba kati ya madai kumi waliyotaka yatekelezwe na Serikali, hakuna hata moja lililofanyiwa kazi.  Hata hivyo,  jana madaktari hao ambao walikaa vikao vya majadiliano na Serikali kwa siku 90 baada ya kusitisha mgomo wao wa pili, wamesema katika madai yao kumi, hakuna hata moja lililotekelezwa na Serikali.  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Stephen Ulimboka jana aliwaeleza waandishi wa habari kwamba ili warejee kazini, Serikali inatakiwa kutekeleza madai yao yote na kusisitiza kwamba dai lao la kwanza ni kuitaka Serikali kuboresha huduma za msingi kwa wagonjwa.  
“Mgomo umeanza jana na hauna kikomo, lengo ni kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yetu, hata zile huduma za dharura nazo kuanzia kesho (leo) zinaweza kusitishwa,” alisema Dk Ulimboka.  Wakati Ulimboka akieleza hayo, huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa (Moi) ilikuwa ikitolewa kwa kusuasua huku baadhi ya wafanyakazi wakisisitiza kuwa mgomo huo upo. 
Licha ya wafanyakazi hao kukiri kuwa siku za mwisho wa wiki idadi ya wagonjwa katika hospitali hizo huwa ndogo, lakini walisisitiza kuwapo kwa mgomo huo na kufafanua kuwa kwa mtu mgeni katika eneo hilo si rahisi kutambua hali hiyo.  Mwananchi Jumapili lilifika katika hospitali hiyo na kukuta huduma zikitolewa ‘kiaina’ huku baadhi ya wagonjwa wakieleza kwamba zimezorota, sio kama siku zilizopita.  
Tamko la Jumuiya      Akieleza kwa kina sababu za mgomo huo, Dk Ulimboka alisema katika madai waliyoyawasilisha, hakuna hata moja lililotekelezwa na kufafanua kwamba Serikali imeongeza dai ambalo wao hawakuliwasilisha.  Madai hayo ni pamoja na kupandishwa kwa ongezeko la mishahara, posho ya kuitwa kazini, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, bima ya afya, nyumba za kuishi, kukopeshwa magari kwa ajili ya usafiri, kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia kazi kwa kupeleka vifaa vya kazi, dawa na kuboresha miundombinu. 
“Serikali imesema imerekebisha viwango vinavyotumika kulipa posho ya uchunguzi wa maiti  kwa Sh 100,000 kwa uchunguzi wa madaktari na Sh50,000 kwa watumishi wengine, lakini hili halikuwa dai letu!” alisema Dk Ulimboka.   Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi aliwatahadharisha madaktari hao kuacha mgomo, akieleza kuwa ni batili na ni kinyume cha viapo vyao vya kazi.  Dk Mwinyi aliainisha mambo 10 ambayo madaktari walikuwa wamepanga kutekelezewa na kusema kuwa kwa sehemu, yametekelezwa na baadhi ya mambo yaliyobakia wanaweza kuyazungumza.

Mwanza
Madaktari zaidi ya 200 waliopo katika Hosptali ya Rufaa ya Bugando jana walianza mgomo rasmi baada ya Serikali kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu madai yao mbalimbali yaliyosababisha madaktari hao kugoma mapema mwaka huu.  Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Mwakilishi wa Kamati ndogo ya kufuatilia madai madaktari hao, Dk Richard Kirita alisema kwamba madaktari wa kada zote katika hospitali hiyo wapo kwenye mgomo isipokuwa baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wakuu wa idara.

 “Kwa kuwa leo sio siku ya kazi unaweza kudhani hakuna mgomo, lakini njoo Jumatatu (kesho) ndo utapata picha halisi ya mgomo kwa sababu wagonjwa watakuwa wengi, lakini hakutakuwa na huduma,”alisema 
Moshi

Hali ya utendaji wa madaktari mkoani Kilimanjaro imeonekana ya kusuasua huku baadhi ya madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC wakisema hawaingii kazini na wengine wakisema bado wanasikilizia.

  Katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi, madaktari waliokuwa zamu walisema kwa leo huwezi kujua aliyeko kwenye mgomo na ambaye hayupo, kwani wengi hawako kazini leo hadi kesho.   B
aadhi ya wagonjwa waliolazwa Hospitali ya KCMC katika wodi ya wanawake, walisema kuwa walitangaziwa kuwa kutakuwa na mgomo wa madaktari na kila mmoja aangalie cha kufanya na kuwa walifika wodini hapo asubuhi na hawakuzungumza na mgonjwa na kutoka.   Wagonjwa hao wamesema Ijumaa jioni wagonjwa wengi waliruhusiwa kuondoka hata kama hali zao hazijatengemaa ambapo walisema wanahofia afya zao kama madaktari watatekeleza msimamo wao.   Mbeya   Katika Hospitali ya Rufaa Mbeya madaktari 10  kati ya 80  ndiyo waliokubali jana kuendelea na  huduma ya kutibu wagonjwa ambapo wengine wameanza mgomo rasmi. 
Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk Eliuter Samky amethibitisha kuwapo na hali ya mgomo na kwamba ana uhakika wa madaktari 10 waliopo zamu kuendelea kazi.    
Awali Mwandishi wa gazeti hili alipofika  katika hospitali hiyo hakukuta daktari yeyote na ofisi za utawala zikiwa zimefungwa huku katika eneo la mapokezi likiwa na wagonjwa ambao wamekaa wakisubiria kupata huduma.  Katika kitengo cha wazazi Meta wanawake wanaokwenda kupata huduma  wamesema wameingiwa na hofu kubwa kwa kukosa huduma hiyo baada ya kuona matangazo yanayosema hakuna mgojwa atakayepatiwa matibabu. 
Wakizungumza hospitalini hapo wanawake hao ambao hawakutaka kuandikwa majina yao, walisema kuwa mbali na kuona tangazo hilo lakini pia waliambiwa na baadhi ya madaktari kuwa ni bora wakaenda sehemu nyingine kwa ajili ya matibabu kwa kile kilichoelezwa kuwa kuwa na wao wapo katika mgomo huo hivyo hakuta kuwa na huduma yeyote kwa mgonjwa.

Arusha
Hali ya mgomo wa madaktari katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, haikuonekana jana asubuhi ingawa katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya madaktari na manesi hawakufika wodimi kuwaona wagonjwa kama wananvyofanya siku nyingine.  
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dk Mlay alipoulizwa na gazeti hili alisema hali hiyo isihusishwe na mgomo uliotangazwa na chama cha madaktari kwa kuwa kimetona na sababu kwamba leo na kesho ni siku za mapumziko .

Baadhi ya wagonjwa na ndugu wanaowauguza walihojiwa na gazeti hili walionyeshwa kushangazwa na hali ya madaktari na manesi kushindwa kuwatembelea leo katika wodi zao kinyume na siku zote.

Mganga Mkuu wa hospitali alisema kwamba hospitalini kwake hakuna mgomo wowote wa madaktari kwa kuwa wanafanya kazi kama kawaida na wala hawatambui suala la mgomo wa madaktari uliotangazwa na Chama cha Madaktari nchini(MAT).
 Tanga  Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo pamoja hospitali nyingine za wilayani jana ziliendelea na  huduma ya kutoa matibabu kwa wagonjwa  kama kawaida.  Katika Hospitali ya Bombo ambayo ni ya Mkoa wa Tanga, Mwandishi wa habari hizi jana alikuta madaktari pamoja na wauguzi waliokuwa zamu wakiendelea na kutoa matibabu kwa wagonjwa waliolazwa pamoja na wale wa kutoka nje. 
Wakizungumza na Mwananchi Jumapili madaktari wa Hospitali ya Bombo walisema wameshindwa kufanya mgomo kwa kuwa hawana taarifa za kuwataka kufanya hivyo bali wamekuwa wakisikia na kusoma kupitia vyombo vya habari.
Haruna Juma ambaye ni mkazi wa Barabara ya 10 Jijini Tanga, aliwashukuru madaktari wa Hospitali ya Bombo kwa kutogoma kwa kuwa mdogo wake anayesumbuliwa na Apendex alipangiwa kufanyiwa upasuaji jana ambapo waganga walimfanyia kama kawaida.  
Waziri
Serikali imesema kuwa itaendelea na msimamo wake ilioutoa bungeni mjini Dodoma wa kuwataka madaktari nchini kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wakati ambapo madai yao ya msingi yakiwa yanashughulikiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro jana baada ya kufanya ziara yake katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, alisema kuwa kimsingi yako mambo ambayo katika mazungumzo na madaktari hao walikubaliana lakini pia yako mambo ambayo hawakukubalina.
Dk Rashid alisema kuwa mambo ambayo walikubalina na madaktari hao yanaendelea kushughulikiwa lakini mambo ambayo walishindwa kukubalina katika baraza la usuluhishi madaktari hao walikimbilia mahakamani ili kutafuta suluhu.
“Na sisi tunasubiri maamuzi ya mahakama kwa hivyo kitendo cha wao kugoma kinakwenda kinyume na sheria kwa kuwa jambo hilo bado halijapatiwa ufumbuzi na mahakama,” alisisitiza.
Katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro hakukuwa na dalili zozote za madaktari na wauguzi kugoma, huduma za matibabu kwa wagonjwa zilikuwa zikiendelea kama kawaida huku baadhi ya wauguzi na madaktari wa hospitali hiyo wakidai kutokuwa tayari kuingia katika mgomo huo.

Amana, Temeke Katika hospitali ya Amana na Temeke  za jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa huduma kama kawaida, isipokuwa Hospitali ya Mwananyamala ambayo kulikuwa na madaktari na waguzi wachache.  Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Meshack Shemwela aliiambia Mwananchi Jumapili jana kwamba huduma ya afya zinaendelea kutolewa kama kawaida na kwamba wanafanya tathmini ilikutambua kama kuna madaktari waliogoma.
Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick alisema kuanzia jana saa 6 usiku walifanya uchunguzi na kubaini kwamba kuna watu waliokuwa wanapita katika kila hosptali kuhamasisha kufanyika lakini madaktari hawajagoma.
Imeandaliwa na  Rehema Matowo,Moshi, Venance George, Morogoro, Burhani Yakub,Tanga, Brandy  Nelson, Godfrey Kahango,Mbeya, Moses Mashalla,Arusha,Sheilla Sezzy,Mwanza Aidan Mhando, Ibrahim Yamola, Geofrey Nyang'oro na Fidelis Butahe,Fidelis Butahe na Geofrey Nyang’oro

June 24, 2012

WEMA AZINDUA SUPER STAR NA OMOTOLA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Omotola akiwasili uwanja wa ndege
hapa akipokelwa na mwenyeji wake Wema sepetu
wema & omotola


June 23, 2012

IKULU: MASHANGINGI SASA BASI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

OFISI ya Rais, Ikulu imesema Serikali itaanza kuwakopesha viongozi wake wa ngazi mbalimbali magari madogo ya gharama nafuu ili waachane na mashangingi yanayotumika sasa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili kuwa mpango huo unaotarajiwa kuanza Julai mwaka huu, una lengo la kupunguza matumizi ya Serikali kwa kuondokana na magari makubwa yenye gharama kubwa za uendeshaji.

Balozi Sefue alisema mpango huo unaanza katika mwaka huu wa fedha ambapo yatachambuliwa magari yanayofaa na yatapendekezwa yatumike katika shughuli gani.

Alipoulizwa kama mabadiliko hayo yatawagusa mawaziri na majaji, Balozi Sefue alisita kulijibu hilo na badala yake alisema kuwa bado suala hilo lipo katika mjadala.

“Hili jambo bado linajadiliwa, haya yote yatafanyika katika mwaka huu wa fedha,” alisema Balozi Sefue. Mwaka wa fedha unaaza Julai mosi mwaka huu.

Akifafanua zaidi alisema, “Kwanza tutatizama gari husika linatumia mafuta kwa kiwango gani, pia tutatizama hata gharama nyingine kama ufundi,” alisema Balozi Sefue.

Alisema kuwa utaratibu huo ukianza viongozi wanaotumia magari ya Serikali wataanza kukopeshwa magari hayo na kupewa posho kwa ajili ya kuweka mafuta.

“Ni kipaumbele cha Serikali kuangalia hilo mwaka huu na hata katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13 imeelezwa wazi, lengo ni kupunguza gharama za uendeshaji,” alisema Sefue.

Aliongeza, “Badala ya kumpa mtu gari tunamkopesha halafu tunakuwa tunampa mafuta ili kupunguza matumizi Serikalini.”

Alisema katika uchambuzi huo wataangalia ni kiongozi gani atahitaji gari la Serikali na yupi atatakiwa kukopeshwa na kwamba hali hiyo itafuatana na kazi za mtumishi husika.

“Tunaangalia hili la magari, lengo ni kuwa na magari ya aina fulani lakini si ya kifahari na tutawakopesha  watumishi,” alisema Sefue.

Alisema kuwa katika uchambuzi huo pia watazingatia ubora wa gari husika ikiwa ni pamoja na kustahimili kusafiri masafa marefu, kulingana na majukumu ya mtumishi.

“Yapo mambo ambayo Serikali imeyapanga na lazima yatekelezwe,” alisema Sefue.

Alipoulizwa kama mpango huo ni utekelezwaji wa mpango uliotolewa na Wizara ya Ujenzi mwaka 2004 wa kubana matumizi ya magari ya Serikali alisema hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Wizara ya Ujenzi yenyewe.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Herbert Mrango alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa mpango huo alisema hawezi kuzungumzia mambo ya Serikali kwenye simu.

Wakati Balozi Sefue akisema hayo tayari kuna baadhi ya viongozi Serikalini wameshajikopesha magari hayo akiwemo Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu.

Suala la Ndulu kujikopesha gari lilielezwa hivi karibuni na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe alipokuwa akisoma bajeti mbadala ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Zitto alisema Serikali inatakiwa kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa kupiga mnada baadhi ya ‘mashangingi’ na kuweka mfumo wa kukopesha magari kwa watumishi wote wa umma wanaostahili magari kama alivyofanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Balozi Sefue alipoulizwa kuhusu suala la Ndulu kujikopesha gari alisema hajuI bali huo unaweza ukawa ni utaratibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT ndiyo ambayo inaweza ikawa imepitisha hilo.
“Kwa maana ya framework hakuna kinachomzuia kufanya hivyo,” alisema.

Katika mkutano wa 7 wa Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo alieleza kuwa kumekuwa na matumizi yasiyo ya lazima katika uendeshaji na ukarabati wa magari hayo na hadi Juni 30, 2010 Serikali ilikuwa inamiliki magari yenye thamani ya Sh5 trilioni.
Alisema mwendelezo wa ununuzi wa magari unaofanywa na Serikali unaongeza gharama za uendeshaji na kusisitiza kwamba matumizi hayo si ya lazima kwa Serikali yenye uchumi mdogo uliozidiwa na madeni.

Mkono: Ufisadi wa Kiwira

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
AELEZA MGODI ULIVYOUZWA BEI YA KUTUPA,NGELEJA NAYE AZUA MTAFARUKU BUNGENI

SAKATA la ufisadi katika uuzwaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya limeibuka upya, safari hii ikielezwa na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kuwa umeuzwa kwa bei ya kutupa.Mbunge huyo ambaye ni mwanasheria, amelitaka Bunge kuunda Kamati Teule kwenda kuchunguza ufisadi huo, huku akihoji sababu za Serikali kuutengea mabilioni ya shilingi wakati umekwishauzwa.

Mkono alisema kuwa, “Mgodi huo wenye thamani ya matrilioni ya shilingi, umeuzwa kwa bei ya kutupa ya dola 700,000 tu za Marekani (Sh1.1 bilioni), kwa kampuni ya Intra Energy ya Australia.”

Mgodi wa Kiwira uliwahi kuzua malalamiko baada ya kumilikishwa kwa Kampuni ya ANBEN Limited, mali ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na mkewe, Anna Mkapa, lakini Januari mwaka huu, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliieleza Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kuwa ANBEN Limited haihusiki tena na mgodi huo.

Alifafanua kuwa kampuni hiyo iliondolewa kuwa miongoni mwa wamiliki wa hisa kwa vile haikuweza kulipia hisa 200,000 ilizokuwa imechukua wakati wa usajili wa Kampuni ya Tan-Power Resources (TPR).

Akichangia mjadala wa Bajeti jana, Mkono alihoji sababu za Serikali kutenga Sh40 bilioni kwa ajili ya kulipa watu wa mgodi wa Kiwira ilhali inajua kuwa mgodi huo uliuzwa kwa bei ya kutupwa tangu mwaka 2007.

“Tumetenga Sh40 bilioni za kuwalipa watu waliotuibia fedha zetu, eti tunasema kwamba tunalipa madeni, haya ni madeni gani ambayo tunakwenda kulipa huko?” alihoji Mkono.

Alisema mwaka 2007 wabunge walipiga kelele wakiitaka Kampuni ya Tan Power iliyokuwa mbia wa Serikali katika mgodi huo, kuurudisha serikalini, lakini mwaka jana kampuni hiyo iliuza mgodi huo kwa bei ya kutupa.

“Unauzaje mgodi huu wenye thamani ya matrilioni ya pesa kwa bei hii ya kutupa?” alihoji na kuendelea, "Haya ni mambo ya ajabu sana. Tungeweza kupata fedha nyingi sana kutokana na mgodi huu na fedha hizi zingetusadia katika kugharimia mahitaji yetu ya bajeti.”

Mbunge huyo aliungana na wabunge wengine kuiponda Bajeti ya Serikali kwa kutegemea fedha za wahisani, huku rasilimali za nchi zikiendelea kufujwa bila huruma.

Alisema nakisi inayoonekana kwenye Bajeti, inatokana na uwezo mdogo wa kukusanya fedha za ndani licha ya kwamba nchi ina utajiri mkubwa wa madini, ambayo hata hivyo, yanawanufaisha watu wengine na kuwaacha Watanzania wakitaabika.

Mkono pia aliishambulia Serikali kwamba ‘ilichakachua’ mradi wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Buhemba na kuwadanganya wananchi ambao hawakunufaika na kitu chochote.

Kutokana na hilo, mbunge huyo alisema kuwa Bajeti ya mwaka 2012/13 imetoa upendeleo kwa baadhi ya maeneo huku ikiyaacha mengine muhimu, ambayo yanagusa masilahi ya wananchi.

“Serikali ilichakachua Buhemba lakini inapeleka tena Sh1 bilioni huko na sijui zinakwenda kufanya nini wakati ingeweza kupeleka katika moja ya shule za jimboni kwangu, au hata kama ingetusaidia wananchi wa Mara kujenga chuo kikuu cha kilimo ambacho kinajengwa mkoani kwetu,’’alisema Mkono.

Alisema yeye binafsi haelewi Serikali inaposema haina fedha kwani migodi ya Kiwira na Buhemba ingetumika vizuri, ingeweza kuipatia Serikali kiasi kikubwa cha fedha kinacholingana na fedha zinazotolewa na wafadhili.

Ngeleja achafua hewa

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja jana alisababisha mvutano mkubwa ndani ya Bunge na kuondoa utulivu kwa muda, kutokana na mchango wake wa kuiponda Bajeti ya Upinzani.

Ngeleja aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini hadi Mei 4, mwaka huu alipong’olewa na Rais Jakaya Kikwete, aliwabeza wapinzani kuwa Bajeti yao ilikuwa imeandaliwa na watu ambao wana maono ya kuandaa bajeti za harusi na maandamano, lakini si katika hali ya kuandaa Bajeti ya nchi kama Tanzania.

“Mheshimiwa Spika, hawa wenzetu walio mbele yangu hawana jipya, na ningependekeza wasimame na kuwaomba radhi Watanzania maana wameandaa bajeti ya maandamano na harusi,’’ alisema Ngeleja.

Alisema Bajeti ya Upinzani ni ya ovyo na haikuainisha vyanzo mbadala vya mapato na hivyo kuwataka Watanzania kuipuuza.

Huku akishangiliwa na mawaziri na wabunge na CCM, alisema kama viongozi wa upinzani wanaitakia mema Tanzania, ni vyema wakatumia nafasi zao ndani ya Bunge kusimama na kuwaomba radhi wananchi kwa kuwa wamesababisha baadhi kutoijali mipango mizuri ya Serikali.

Hali hiyo ilisababisha wabunge wengi wa Chadema kusimama na kuomba Mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee walipewa nafasi ya kuzungumza, huku Ngeleja akipinga kila kitu walichosema.

Mdee alimweleza Spika kuwa tatizo la Ngeleja siyo kupingana na maoni ya Kambi ya Upinzani bali ni hasira za kuondolewa katika nafasi ya uwaziri wa Nishati na Madini, jambo ambalo bado linamuuma.

“Mheshimiwa Spika, hakuna kitu kama hicho, tatizo la Ngeleja ni kuondolewa katika nafasi ya uwaziri na siyo kitu kingine, maana kama ni maneno ambayo yalikuwa yamekosewa tayari tulishaleta mabadiliko yake humu ndani,” alisema Mdee, kisha akakubaliana na Spika, kuondoa maneno kuwa tatizo la Ngeleja ni uwaziri.

Kwa upande wake Mbowe, alisema kuwa Ngeleja hakusoma bajeti yao vizuri na kumwomba Spika kutoa tamko la namna ya kuwashughulikia wote wanaodanganya umma katika michango yao.

Lissu alitoa ufafanuzi ulioafikiwa na Spika, kuwa Bajeti inayojadiliwa bungeni ni moja ambayo ni ya Serikali, na kwamba Kambi ya Upinzani haina ya kwake, bali inatoa maoni kwa ile ya Serikali.

Chanzo cha habari: Mwananchi

MADAKTARI WATANGAZA MGOMO KESHO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
JUMUIYA ya Madaktari imetangaza rasmi kuanza kwa mgomo usio na kikomo kuanzia kesho, huku ikidai Serikali imekataa kutekeleza madai yao yote yaliyowasilishwa katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Wakati madaktari hao wakitangaza kurejea rasmi katika mgomo huo uliositishwa miezi mitatu iliyopita, Pinda aliliambia Bunge jana wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, kuwa mgomo huo ni batili na haukubaliki.

Saa chache baada ya Pinda kutoa onyo hilo lililorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na redio kutoka Dodoma, madaktari hao wakiwa jijini Dares Salaam walitangaza mgomo huo wenye lengo la kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao.

Mgomo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari na Dk Stephen Ulimboka, muda mfupi baada ya kukamilika kwa mkutano wa ndani wa madaktari, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Utamaduni la Watu wa Urusi.

Dk Ulimboka alisema mgomo huo usio na kikomo utawahusu madaktari wa kada zote nchini, na unatarajiwa kuanza kesho, baada ya wiki mbili walizotoa kwa Serikali kumalizika bila ya makubaliano yoyote.

“Madaktari kwa ujumla wao wamekubaliana kuwa watarejea katika mgomo usio na kikomo, hii ni kutokana na kugundua kuwa hakuna dhamira ya dhati ya Serikali, kumaliza mgogoro kati yetu na Serikali, uliodumu kwa muda mrefu sasa,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza,

“Serikali imetupilia mbali madai yote yaliyofikishwa katika meza ya majadiliano baina ya wawakilishi wa Serikali na madaktari na taarifa iliyotolewa bungeni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na pia majibu ya Waziri Mkuu leo, yamepotosha kila kilichomo katika taarifa tuliyonayo sisi.”

Alifafanua kwamba Serikali imetupilia mbali madai yote ambayo kabla ya kukubali kurudi katika meza ya majadiliano yalionekana kuelekea kupata mwafaka.

Dk Ulimboka alisema kuwa kauli iliyotolewa na Pinda bungeni, kwamba walikubaliana, si ya kweli na hata posho zilizotajwa kwenye taarifa za kamati hiyo ni za dharura kabla ya kuanza kwa vikao vya majadiliano.

Alisema msimamo wao ni kuanzisha mgomo usio na kikomo na hakuna njia ya mkato ya kuuzuia, njia pekee ni Serikali kurudi katika meza ya majadiliano.

Kuhusu ushauri uliotolewa na Pinda kuwataka waende mahakamani, Dk Ulimboka alisema jumuiya yao haiko tayari kwenda na kwamba itaendelea na utaratibu wake wa kushinikiza madai hayo kwa njia ya mgomo.

“Sisi hatuendi mahakamani na hakuna njia yoyote ya kuuzima mgomo zaidi ya kurudi kwenye meza ya majadiliano yenye lengo la kufikia mwafaka wa yale tunayotaka kukubaliana," alisisitiza.

Alisema katika madai yao ya msingi waliyotoa serikalini, hadi sasa limetekelezwa moja tu, huku wakishangazwa na Serikali kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti kutoka Sh10,000 za awali hadi Sh100,000 kwa madai kuwa posho hiyo haikuwa miongoni mwa madai yao.

“Sisi katika madai yetu hatukuliweka dai hili la posho ya uchunguzi wa maiti, kwa sababu hilo siyo dai letu la msingi. Kazi ya uchunguzi wa maiti siyo ya kila wakati, hufanywa tu pale watu wanapokuwa na mashaka na kifo cha mtu husika, lakini pia haifanywi na madaktari wote,” alisema Dk Ulimboka.

Madai ya madaktari

Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitega alitaja madai yaliyowasilishwa katika kamati hiyo kuwa ni hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini, ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za kuitwa kazini.

Akizungumzia dai la hali bora ya mazingira ya kazi, alisema hadi sasa hakuna kilichotekelezwa huku hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa ikizidi kuwa mbaya.

“Tunaweza kusema tangu tukubali kuingia kwenye meza ya majadiliano hali imezidi kuwa mbaya. Katika hospitali kubwa kama Muhimbili inakosa vitendea kazi, dawa, wagonjwa kulazwa chini huku rufaa za wagonjwa kwenda nje ikiongezeka,” alisema Dk Chitega na kuongeza:

“Tunachotaka sisi ni huduma za afya ziboreshwe ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora za afya na kupunguza rufaa za kwenda nje kutibiwa.”

Dk Chitega alitoa mfano wa gharama zilizotumika kwa mwaka wa fedha wa 2010/11, kuwa ni Sh7 bilioni, ilhali fedha zilizotumika kwa kipindi cha mwaka huu kwa ajili ya uendeshaji hospitali kubwa sita za hapa nchini kuwa Sh5 bilioni.

“Tulipendekeza pia mchakato wa rufaa uboreshwe kwa kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje kwa kuboresha huduma za ndani, Serikali ilianzisha Taasisi ya Mifupa (MOI), ikapeleka madaktari kwenda kusoma India, wamekuja kufanya kazi wamekosa vifaa wameondoka. Sisi lengo letu ni kuona fedha za nchi zinatumika kuwasaidia Watanzania,” alisema Chitega.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Godbles Charles alisema taarifa zilizotolewa bungeni na Pinda na Dk Mwinyi zimepotoshwa na zina lengo la kuwarejesha kwenye mgomo.

Pinda awaonya

Mjini Dodoma, Pinda alitoa taarifa jana kwamba suala hilo liko Mahakama ya Kazi na kuonya kwamba mgomo huo ni batili, wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Mbowe alitaka kujua hatua zilizofikiwa na Serikali katika kutatua mgogoro wa madaktari na walimu nchini, na sababu za kutotekelezwa makubaliano yaliyofikiwa katika majadiliano.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema Serikali iliunda tume kushughulikia mgogoro wa madaktari ambapo kulikuwa na madai 10 yaliyojadiliwa na kati ya hayo, madai matano yalifikiwa mwafaka na madai mengine matano bado yanaleta mvutano.

“Ni kweli tumekuwa na mgogoro na madaktari lakini tumekuwa tukizungumza nao kwa kipindi chote cha tatizo hili, ili kupata mwafaka na kwa kama mwezi mmoja tume iliyoundwa ilimaliza kazi na kuwasilisha taarifa serikalini kwa ajili ya kufikia maamuzi,” alisema Pinda.
 
Pia alisema Dk Mwinyi alijitahidi kuonana na madaktari lakini haikuwezekana, ndipo akamshauri awaandikie barua ambayo madaktari walimjibu kuwa, hawaoni haja ya kuendelea na mazungumzo, kwani wamekuwa wakifanya kwa karibu miezi mitatu bila mafanikio.

Waziri mkuu alisema, baada ya Serikali kufikia hatua hiyo, ikaona ni vyema sasa irudi kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa kuwa hawakuafikiana.

Alisema kwenda CMA si mara ya kwanza, kwani awali walikwenda lakini Serikali ikashauri ni kwa nini wasijadiliane nje na kufikia mwafaka, na baadaye kurudi CMA ili kuandikisha makubaliano waliyofikia.

“Hivyo tumerudi tena CMA kutoa taarifa na sasa suala hili limepelekwa mahakamani, lakini kama Jumamosi wakianza mgomo ni kinyume cha sheria… mimi nina wasihi sana, bado ipo nafasi ya kufikia mwafaka,” alisema Pinda.

Alisema mambo matano ambayo wamefikia mwafaka ni kuongeza malipo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu kwa madakari ambapo wasaidizi sasa watalipwa Sh50,000 na madaktari Sh100,000.

Pia alisema Serikali ilikubali kuwaondoa mawaziri na watendaji wengine wa wizara hiyo, imeongeza malipo ya kuitwa kwa dharura na mengine kadhaa.

Waziri Mkuu alisema mambo ambayo hawajafikia mwafaka ni pamoja na ongezeko la mishahara ya madaktari, posho ya usafiri na nyumba na  posho za kufanya kazi katika mazingira magumu.

Mgogoro wa walimu

Kuhusu walimu, Pinda alisema hatua iliyofikiwa hivi sasa ni nzuri kwani tayari chombo cha majadiliano ambacho kilikuwa bado, sasa kimeundwa.

Alisema tayari Katibu Mkuu, Utumishi, amempatia taarifa za kukamilika kwa chombo hicho ambacho sasa kitawezesha kufikiwa makubaliano ya msingi na hivyo kutatua matatizo ya walimu.

Waziri Mkuu, alitoa angalizo kutokana na ujumbe wa simu unaosambazwa, ambao hata hivyo hakuufafanua, na kuomba kusiharakishwe kufikia huko kwani baada ya muda mfupi mwafaka wa madai ya walimu utapatikana.

Ujumbe huo ambao umesambazwa katika mitandao ya kijamii, unasomeka: “Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa TZ (Tanzania); (Ajira mpya cheti) mwalimu Sh244,400, Afya Sh472,000, Kilimo/Mifugo Sh959,400, Sheria Sh630,000.
Diploma: Mwalimu Sh325,700,  Afya Sh682,000, Kilimo/Mifugo Sh1,133,600, Sheria Sh871,500.

“Degree (shahada) Mwalimu Sh469,200, Afya Sh802,200, Kilimo/Mifugo Sh1,354,000,  Sheria Sh1,166,000. Je upo tayari kuvumilia kunyanyaswa hivyo katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Ungana na CWT kudai nyongeza ya mishahara 100%, Teaching allowance (posho ya kufundisha), hardship allowance (posho ya mazingira magumu). Wape sms hii walimu 20 tu! Mshikamano daima.”


Chanzo cha habari: Mwananchi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat